• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
WALIOBOBEA: Muthaura alichapa kazi akaaminiwa na Kibaki

WALIOBOBEA: Muthaura alichapa kazi akaaminiwa na Kibaki

KWA HISANI YA KENYA YEAR BOOK

MAJINA ya wanaume na wanawake waliofanikisha utawala wa miaka kumi wa Rais Mwai Kibaki yanapotajwa, jina la Francis Kirimi Muthaura, aliyekuwa Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri linajitokeza kwa nguvu.

Akiwa mtumishi wa umma aliyekuwa na uzoefu mkubwa, Muthaura alileta ujuzi muhimu wa kiuchumi, Sayansi ya siasa, kibalozi na kiutawala. Katika serikali ya Kibaki, Muthaura alikuwa

Sally Kosgei, alivyokuwa katika serikali ya Kenya African National Union (KANU). Hadi wakati huu, Kosgei ndiye mwanamke wa pekee kuhudumu katika wadhifa huo tangu Kenya ilipopata uhuru.

Muthaura alisimamia operesheni za Kibaki; alikuwa kiunganishi kati ya Rais na mawaziri.

Alisimamia Baraza la Taifa ya Ushauri wa Usalama, jambo ambalo lilimpatia fursa ya kupata habari za ujasusi kuhusu usalama wa taifa. Akiwa mwenyekiti wa kundi la makatibu wa wizara, aliongoza mazungumzo mengi kuhusu sera. Hii inaeleza jukumu lake katika uundaji na utekelezaji wa mikakati ya sera za serikali ya NARC.

Kwenye chapisho lenye dibaji Three Key Lessons on Growing the Economy from Kenya’s Vision 2030, Muthaura alieleza kilichofanya serikali ya Kibaki kufufua uchumi wa Kenya.

Alieleza kwamba Ruwaza ya 2030 ilikuwa sehemu ya Mpango wa Ufufuzi wa Uchumi kufanikisha Ajira na Kubuni Utajiri.

Kufaulu kwa utekelezaji wa mpango huo, uliokuwa mwongozo wa uchumi wa serikali ya NARC, kulichochea kubuniwa kwa ruwaza hiyo.

Alisema Ruwaza ya 2030 ilikuwa mkakati wa NARC wa kuondoa utamaduni wa mipango ya serikali kudumu kwa miaka mitano.

Baadhi ya miradi na mipango iliyolengwa katika Ruwaza ya 2030 ilikuwa ni katika sekta za Kilimo, Utalii, Viwanda, Huduma za Fedha, barabara, kawi, na elimu.

Ruwaza hiyo pia ilieleza mipango ya serikali ya Kibaki katika afya na makao, Lapsset ( mradi wa uchukuzi wa Bandari ya Lamu- Sudan Kusini- Ethiopia) Konza City, Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta, Reli ya Kisasa, Bandari ya Mombasa na Maeneo Spesheli ya Uchumi.

Baada ya kura ya maamuzi ya katiba ambayo upande wa serikali ulishindwa 2005, Kibaki alitimua mawaziri wote ikiwa mara ya pekee katika historia ya Kenya ambapo Rais alifuta baraza nzima la mawaziri kwa wakati mmoja. Katika serikali ya muungano baada ya ghasia za uchaguzi mkuu wa 2007, Muthaura alitekeleza jukumu muhimu akiwa mkuu wa utumishi wa umma na katibu wa baraza la mawaziri.

Muthaura ana tajiriba pana ya masuala ya diplomasia. Alikuwa balozi wa Kenya katika nchi za Ubelgiji, Luxembourg na Muungano wa Ulaya. Amekuwa balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa, New York. Kati ya Machi 1996 na Aprili 2001 alikuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Anataja Rais Kibaki kama kiongozi mnyenyekevu aliyejitolea kuhudumia Kenya.

Kulingana na Muthaura, ghasia za baada ya uchaguzi mkuu za 2007-2008 hazikufaa kutokea; anaamini kwamba zingeepukwa.

Muthaura anabaki Mkuu wa Utumishi wa Umma na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa pili kuhudumu muda mrefu baada ya Geoffrey Kariithi, aliyehudumu kwa miaka 13. Kwa wakati huu anasimamia Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru Kenya.

You can share this post!

Kalonzo hatimaye ajiunga na Raila dakika za mwisho

Bayern na Hoffenheim nguvu sawa katika Bundesliga

T L