• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
CECIL ODONGO: Unafiki mkubwa kwa Kenta, Khalwale kuvumisha wawaniaji wa vyama vingine

CECIL ODONGO: Unafiki mkubwa kwa Kenta, Khalwale kuvumisha wawaniaji wa vyama vingine

NA CECIL ODONGO

HATUA ya baadhi ya viongozi wa kisiasa kugeuza mkondo na kupigia debe viongozi wa chama au mrengo pinzani kwa ajili ya kupata vyeo wanavyowania ni unafiki mkubwa na ukosefu wa uaminifu.

Wiki hii, Mbunge wa Kajiado Kaskazini, Moitalel Ole Kenta alinukuliwa kwenye mkutano wa kampeni ya Narok, akiwarai baadhi ya wapiga kura wajiamulie ni nani watakayempigia kura kwa wadhifa wa Urais ila wampe kura za ugavana.

Bw Kenta ambaye amehudumu kama mbunge kwa mihula miwili anasaka kiti cha ugavana wa Narok kwa tikiti ya ODM.

Alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa kampeni upande unaopakana na inakoishi jamii ya Kipsigis ambayo inaunga mkono Naibu Rais Dkt William Ruto.

Aidha, baadhi ya viongozi wa Jubilee katika eneo la Mlima Kenya nao wamekuwa wakiendeleza kampeni za kuwaomba raia wawapigie kura kivyao badala ya kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga ambaye anaungwa mkono na chama hicho.

Majuma machache yaliyopita, aliyekuwa Seneta wa Kakamega Bonny Khalwale nusra akabane koo na seneta wa Kakamega Cleophas Malala ambaye anawania Ugavana.

Wawili hao wapo katika mrengo wa Kenya Kwanza ila Bw Khalwale alionekana kumpigia upato mwaniaji wa ugavana wa ODM, Fernandes Barasa.

Je, kutakuwa na manufaa gani ya kutumia vyama vya kisiasa au umaarufu wao kuwania vyeo mbalimbali ilhali wanasiasa wanaofaa kuvivumisha hawadhihirishi uaminifu kwa vyama hivyo?

Iwapo una imani katika utendakazi wa chama cha kisiasa, basi kama kiongozi lazima uwe na ujasiri wa kukitetea na kukitumia kuuza ajenda yako hata ukikabiliwa na upinzani wenye uzito.

  • Tags

You can share this post!

Romelu Lukaku arejea Inter Milan kwa mkopo baada ya kuagana...

TUSIJE TUKASAHAU: Chokoraa wangali tishio jijini

T L