• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:50 AM
DARUBINI YA UKWELI: Atwoli anapotosha kudai Ruto amepandisha bei ya mafuta

DARUBINI YA UKWELI: Atwoli anapotosha kudai Ruto amepandisha bei ya mafuta

KATIBU Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini (COTU) Francis Atwoli hivi majuzi alidai kuwa bei ya juu ya mafuta humu nchini imesababishwa na Naibu wa Rais William Ruto pamoja na washirika wake.

Bw Atwoli alimtaka Dkt Ruto kutoumiza Wakenya kwa kupandisha bei ya mafuta kupata fedha za kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9.

Mamlaka ya Kudhibiti Petroli na Kawi nchini (Epra) ilipovunja rekodi kwa kuongeza bei ya mafuta kwa Sh9 wiki iliyopita, ilisema kuwa hali hiyo ilichangiwa na kudorora kwa thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya dola ya Amerika.

Mamlaka hiyo pia ilisema bei ya mafuta ghafi imekuwa ikiongezeka tangu wanajeshi wa Urusi walipovamia Ukraine Februari 24, 2022.

Urusi inaongoza kwa kuuza mafuta katika soko la kimataifa duniani.

Uamuzi: Madai ya Atwoli yanapotosha

  • Tags

You can share this post!

Bodaboda anayedaiwa kuua rafikiye anyakwa na kuzuiliwa

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Siaya

T L