• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Siaya

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Siaya

NA KASSIM MWALIMU

SIAYA imejulikana kuwa nyumbani kwa watu mashuhuri kama; aliyekuwa makamu wa rais wa kwanza nchini Jaramogi Oginga Odinga, aliyekuwa rais wa kwanza wa Marekanai mwenye asili ya Afrika Barrack Obama, aliyekuwa wakili wa kwanza nchini Kenya Argwings Kodhek, waziri wa Elimu wa sasa Profesa George Magoha, na Mkenya wa kwanza kupata shahada ya digrii Profesa David Wasawo.

Fauka ya hayo kaunti ya Siaya inajulikana kuwa na maeneo ya kitalii kama Ziwa Kanyaboli, na chemichemi ya maji ya Yala.

CHANGAMOTO: Idadi kubwa ya vijana wasio na ajira na wengi wanaishi kwa bajeti ya chini ya Dola moja kwa siku.

Wawaniaji wa Ugavana

James Orengo ambaye kwa sasa amehudumu kama mbunge wa Ugenya kwa miaka kumi na minane na seneta wa Siaya kwa mwongo mmoja.

Alihitimu kama wakili katika Chuo Kikuu cha Nairobi 1974.

Alichaguliwa kama mbunge kwa mara ya kwanza 1980 katika eneobunge la Ugenya.

Nicholas Gumbo alikuwa mbunge wa Rarieda kwa muda wa miaka kumi, 2007-2017, ambapo alijitosa kuwania kiti cha ugavana. Ni mhandisi umeme (electrical engineer) aliyehitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi 1989.

Millicent Oduor ni Mwanasaikolojia. Ana shahada ya digrii katika taaluma ya Nasaha ya Udadisi Nafsia (Counselling Psychology) kutoka Chuo Kikuu cha Catholic University.

William Ochieng, 36 ni mkereketwa wa masuala ya spoti. Kwa sasa ni mwakilishi wa shirika la kandanda nchini, FKF katika utanzu wa Siaya. Ana shahada ya digrii ya Fizikia kutoka Chuo Kikuu cha Jomo Kenyatta (JKUAT). Alihitimu 2009.

Wawaniaji wa Ubunge

ALEGO USONGA – Samuel Atandi (ODM), Muluan Omondi (DAP-K) na Sospeter Aming’a (Huru).

UGUNJA – Opiyo Wandayi (ODM), Oyugi Dor (UDM) na Francis Odawa wa MDG.

GEM – Elisha Odhiambo (ODM), Isaiah Ndiege (DAP-K), Winnie Auma (MDG) na Adino Dan Odhiambo.

RARIEDA – Otiende Amolo (ODM) na Netto Adhola (UDM)

UGENYA – David Ochieng (MDG) na Dkt Daniel Odhiambo (ODM)

BONDO – Gideon Ochanda (ODM), Kendrick Namal Orony (UDA), Humphrey Opondo Osuo (Huru), Noah Migudo Winja (Huru) na Kuyo John Barack (TPS)

Wawaniaji wa Kiti cha Mwakilishi wa Kike

Dkt Christine Ombaka wa ODM amehudumu kwa kiti hicho kwa muda wa mwongo mmoja. Kabla ya kijitosa ulingoni mwa Siasa alifunza katika Chuo Kikuu cha Maseno.

Mildred Ogogo amekuwa katika siasa za muungano wa waalimu wa KNUT kama mwakilishi wa kike katika kaunti ya Siaya. Kitaaluma yeye ni mwalimu.

Sella Ayimba ni mwanahabari ambaye alikuwa akifanya katika redio ya Nam Lolwe. Ana shahada ya digrii katika taaluma ya Uanahabari.

Maslister Akinyi Oudia ni mwalimu wa chekechea (ECDE). Ana digrii katika ECDE. Kwa sasa alijiuzulu kazi hiyo ili kuingia katika siasa.

 

  • Tags

You can share this post!

DARUBINI YA UKWELI: Atwoli anapotosha kudai Ruto...

Maseneta waidhinisha pendekezo la serikali kupandisha...

T L