• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
KINYUA BIN KING’ORI: Utepetevu wa IEBC wakeketa maini tukielekea uchaguzini

KINYUA BIN KING’ORI: Utepetevu wa IEBC wakeketa maini tukielekea uchaguzini

NA KINYUA BIN KING’ORI

HUKU Wakenya wakitarajia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuwaelezea mikakati iliyobuniwa kufaulisha zoezi la uchaguzi wa Agosti 9, 2022, inashangaza kwamba, tume hiyo iliwapa vyeti vya uteuzi baadhi ya wawaniaji wa nyadhifa za ugavana ambao hawana shahada kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa nchini.

Je, iweje wanasiasa wenye shahada ghushi waidhinishwe kuwania nyadhifa za kisiasa na uongozi?

Je, asasi zinazofaa kutathmnini uhalali wa stakabadhi muhimu za kila mgombeaji zilikuwa wapi wanasiasa wajanja wakiwasilisha shahada feki kwa IEBC?

Kesi za wanasiasa hao zinashughulikiwa na jopo la kutatua mizozo ya uchaguzi chini ya himaya ya wakili mwenye upevu mkuu, Wambua Kilonzo.

Tunayo imani kesi hizo zitashughulikiwa kwa haki bila kujali mirengo ya kisiasa au kuingiliwa na watu wenye ushawishi serikalini kuhangaisha wanasiasa wa mrengo mmoja.

Wanajopo hao ni watu shupavu wanaoweza kuelewa ukweli na siasa ili waweze kusaidia IEBC kupata imani kwa Wakenya.

Ukweli mchungu ni kwamba, baadhi ya maamuzi ya IEBC, hasa yanayotolewa na mwenyekiti wake Bw Wafula Chebukati yanaonyesha ulegevu, upungufu au udhaifu katika tume hiyo.

Kuidhinishwa kwa wawaniaji wenye vyeti ghushi na hulka zinazotiliwa shaka ni kudunisha hadhi ya tume hiyo na pia kuthibitisha bado haikuwa imefanyia mageuzi sheria zake kikamilifu na huenda Wakenya watakosa imani na kukosa kuamini matokeo ya tume hiyo baada ya kupiga kura.

Kuidhinisha mtu ambaye hana digrii kuwania ugavana kaunti kama vile Nairobi, Mombasa, Taita Taveta, Makueni na kadhalika ni sawa na kudharau wananchi wa maeneo hayo.

 

  • Tags

You can share this post!

Jaji akosoa uzuiliaji washukiwa seli muda mrefu

Kingi atumai Ruto hatamruka akishinda urais

T L