• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 12:38 PM
TAHARIRI: Usahihishaji wa KCPE uzingatie haki za walimu

TAHARIRI: Usahihishaji wa KCPE uzingatie haki za walimu

NA MHARIRI

BAADA ya kukamilika kwa mtihani wa kitaifa wa Darasa la Nane (KCPE), sasa macho yote ni kwa shughuli ya usahihishaji na hatimaye matokeo.

Tayari waziri wa Elimu Profesa Gaorge Magoha ametangaza kwamba usahihishaji wa mtihani huo umeanza.

Watahiniwa watatarajia kujua majibu ndani ya wiki mbili zaijazo. Hii ina maana kuwa kila mmoja kati ya watahiniwa milioni moja na laki mbili waliomaliza mtihani jana, atakuwa amejua alama zake.

Usahihishaji huu wa haraka ni jambo jema. Miaka ya nyuma, ucheleweshaji matokeo ulitoa fursa ya ukarabati, ambapo watu walio na uwezo kifedha au kisiasa walishawishi matokeo ya mwisho.

Kunapokuwa na haraka ya kuwapa matokeo wanafunzi, mara nyingi watu hupokea matokeo hayo wakiwa bado wana hamu ya kuyafahamu.

Hata hivyo, katika uharakishaji huo, Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) na wizara ya Elimu, zihakikishe hakuna ukiukaji wa haki za binadamu. Miaka miwili iliyopita, walimu walilalama kufanyishwa kazi kama maroboti. Ilidaiwa wakati huo kwamba walikuwa wakilazimishwa kukesha wakisahihisha, ili wakamilishe kazi hiyo ndani ya muda uliotengwa.

Wizara na KNEC zinapaswa kufahamu kwamba Kenya haiendi popote. Hata kama ni muhimu kutangaza matokeo haraka, maslahi ya watoto yasiwe muhimu kushinda ya walimu. Kumfanyisha kazi Mwalimu kama punda, ni ukiukaji wa kanuni za Leba.

Mwalimu aliyepewa muda wa kutosha, atasahihisha kwa makini. Atasoma kila neno lililoandikwa na kutoa alama kwa mtahiniwa bila ya kuathiriwa na uchovu, usingizi au hisia za kuwa anateswa.

Hizi fikira kwamba ni heri punda afe lakini mzigo ufike, zimepitwa na wakati. Ni sharti wanaosimamia usahihishaji wawe na utu na wate fursa kwa walimu kufanya kazi yao kwa mujibu wa kauni zinazoongozwa maslahi ya wafanyikazi.

Kwa kuwa mpango wa serikali ni kila mtahiniwa kijuinga na shule za upili, kuwe na mipango ya mapema kuwatambua wazazi wasio na mapato.

Shule zitafunguliwa wiki ya mwisho ya mwezi Aprili na pengine wiki moja baadaye wazazi watakaokuwa wamelipia karo watoto walio sekondari, watatarajiwa kulipia watakaojiunga na Kidato cha Kwanza.

Mpango wa kuwasaidia watoto werevu kutoka familia zisizojiweza, wapaswa kuanza kazi punde tu matokeo yanapotangazwa, ili kusiwe nah ali ambapo hata muhula wa kwanza unapoisha, baadhi ya watoto werevu huwa wangali nyumbani.

You can share this post!

Mshukiwa ambaye alichomoa pingu na kuhepa polisi asakwa

KINYUA BIN KING’ORI: Mikataba yote baina ya wanasiasa...

T L