• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 10:50 AM
KINYUA BIN KING’ORI: Mikataba yote baina ya wanasiasa iwekwe wazi kwa wapiga kura

KINYUA BIN KING’ORI: Mikataba yote baina ya wanasiasa iwekwe wazi kwa wapiga kura

NA KINYUA BIN KING’ORI

WANASIASA wakuu nchini wanaowania urais kwa sasa wako katika harakati za kuunda miungano ya kisiasa kwa kutia saini Miktaba ya Maelewano inayoelezea jinsi watakavyoshirikishwa au kushirikiana katika kuunda serikali katika kipindi cha miaka mitano ijayo ikiwa mgombeaji wao ataibuka mshindi uchaguzini.

Lakini imekuwa kama mazoea kwa wanasiasa wetu kusalitiana na visa vya viongozi kukosa kutimiza ahadi zao. Hali hiyo imekuwa ikisababisha kuvunja kwa miungano hiyo. Umewahi kujiuliza, je, kwa nini viongozi wamezoea kusalitiana kwa kukosa kuheshimu makubaliano ya awali kisiasa ?

Kwa nini Rais Uhuru Kenyatta ameruka Naibu wake Dkt William Ruto na badala ya kuzingatia ahadi yake kwa Dkt Ruto, sasa ndiye yuko kwenye mstari wa mbele kushabikia aliyekuwa hasimu na mpinzani wake mkuu Raila Odinga?

Je,ulisikia Kalonzo Musyoka akifichua amesalitiwa na kiongozi wa ODM Raila Odinga kwa kukosa kutimiza ahadi ya kumuunga mkono 2022?.

Mada hii leo imevutiwa na madai ya Bw Musyoka kwamba, katika uchaguzi wa 2017, alikuwa ameweka mkataba wa makubaliano na Bw Odinga ambao ulikuwa ubakie siri.

Kulingana na makubaliano hayo, Kalonzo angeungwa mkono na Raila mwaka huu, baada ya yeye kumuunga mkono katika uchaguzi uliopita.

Lakini leo, Bw Odinga ameidhinishwa na chama Cha ODM na anatarajiwa kuwania Urais kupitia muungano mpya wa Azimio la Umoja.

Ili kuwe na uwazi na kuzidisha imani ya makubaliano ya kisiasa kutimizwa siku za usoni, mikataba hiyo haipaswi kuundwa katika mazingira ya kisiri,bali kwa kushirikisha wanachama wa vyama vya kisiasa husika.

  • Tags

You can share this post!

TAHARIRI: Usahihishaji wa KCPE uzingatie haki za walimu

VALENTINE OBARA: Mila, itikadi zinazokandamiza akina mama...

T L