• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Bila sare rasmi na beji, ni vigumu raia kujua huyu ni polisi au mkora

TUSIJE TUKASAHAU: Bila sare rasmi na beji, ni vigumu raia kujua huyu ni polisi au mkora

KUTOKANA na uwezekano wa kutokea kwa visa vingi vya uhalifu msimu huu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya, idadi ya maafisa wa polisi wanaoshika doria za usalama imeongezeka mjini na vijijini.

Lakini imekuwa vigumu kwa Wakenya kuwatambua baadhi ya maafisa na kuwatofautisha na wakora ambao hujifanya kuwa maafisa wa polisi na kuwaibia raia.

Hata hivyo, ikumbukwe kwamba alipokuwa akipigwa msasa na Kamati ya Bunge kuhusu Usalama mnamo Novemba 11, 2022 katika ukumbi wa County Hall, Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome aliahidi kuhakikisha kuwa maafisa wa polisi wanavalia sare zao wakiwa kazini.

Aidha, aliwaahidi wanachama cha kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Narok Magharibi Gabriel Tongoyo, kwamba atahakikisha kuwa maafisa wote wanavalia beji zenye majina na nambari zao za kazi nyakati zote wakiwa kazini ili raia wawatambue kwa urahisi.

Lakini Dkt Koome hajatimiza ahadi hiyo kwamba wengi wa maafisa wa polisi bado wanaendesha doria za usalama wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia.

Inakuwa vigumu kwa raia kutofautisha kazi ya wakora na maafisa halali wa polisi. Kuna hatari kwamba wakora watawahangaisha na kuwaibia raia wakati kama huu wakijifanya kuwa maafisa wa polisi.

You can share this post!

Misongamano yatatiza maelfu wakienda vijijini

Rais Ruto na mkewe kusherehekea Krismasi nyumbani Sugoi

T L