• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Dkt Ruto atuambie mradi wa kiwanda cha mbolea umefikia wapi

TUSIJE TUKASAHAU: Dkt Ruto atuambie mradi wa kiwanda cha mbolea umefikia wapi

AKIENDESHA kampeni zake katika kaunti za Magharibi ya Kenya na Trans Nzoia mwishoni mwa wiki iliyopita, Naibu Rais William Ruto aliahidi kupunguza gharama ya pembejeo za kilimo, miongoni mwa changomoto nyingine zinazowasibu wakulima.

Kwa mfano, ameahidi kupunguza bei ya mbolea ya upanzi kutoka Sh6,000 hadi Sh2,500 kwa gunia moja la kilo 50, akishinda urais mnamo Agosti 9.

Dkt Ruto alisema kuwa hiyo ni sehemu ya mpango wake wa kuimarisha uzalishaji wa chakula nchini.

Lakini Naibu Rais asije akasahau kuwa mnamo Machi 4, 2014 aliahidi kuwa serikali ya Jubilee ingeshirikiana na nchi ya Japan, kuanzisha kiwanda cha kutengeneza mbolea nchini ili kuondoa utegemezi wa bidhaa hiyo inayoagizwa kutoka nje.

Akiongea mjini Eldoret wakati huo, Dkt Ruto, ambaye amewahi kuhudumu kama Waziri wa Kilimo, alisema kuwa ujenzi wa kiwanda hicho ungeanza mwaka huo na kukamilika 2017.

Aliongeza kuwa baada ya kukamilishwa kwa ujenzi wa kiwanda hicho bei ya mbolea inayotumika katika upanzi wa mahindi ingeshuka kutoka Sh3,500 wakati huo hadi Sh1,200 kwa gunia moja la kilo 50.

Lakini kufikia sasa Dkt Ruto hajaelezea ni kwa nini mradi huo ulikwama.

  • Tags

You can share this post!

Veemisc ni mwanamuziki anayefanya vizuri pia katika...

Kalonzo kupewa mwelekeo baada ya matokeo ya kamati ya Azimio

T L