• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 10:30 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Japhet Koome hajabuni Mamlaka ya Usalama ya Kaunti

TUSIJE TUKASAHAU: Japhet Koome hajabuni Mamlaka ya Usalama ya Kaunti

WANANCHI katika maeneo ya kadha nchini haswa North Rift na Kaskazini Mashariki na Pwani wanaendelea kuathiriwa na visa vya utovu wa usalama.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari, shule kadha katika kaunti za Elgeyo Marakwet, Baringo na Lamu hazijarejelea shughuli za masomo wiki moja baada ya shule zote nchini kufunguliwa rasmi mnamo Januari 23, 2023.

Serikali haijafaulu kurejesha usalama katika maeneo licha haya Waziri wa Usalama Kithure Kindiki kuzuru maeneo athirika kila mara na kusajili Polisi wa Akiba (NPR) kusaidiana na polisi kupambana na wahalifu.

Lakini ikumbukwe mnamo Novemba 8, Inspekta Jenerali Mpya wa Polisi Japhet Koome aliahidi kubuni Mamlaka ya Usalama ya Kaunti (CPA) katika kaunti zote 47 nchini, akianza na Nairobi.

“Baada ya kubuni mamlaka ya kusimamia usalama katika kaunti ya Nairobi, nitabuni mamlaka hizo katika kaunti zingine 46 zilizosalia,” akasema kwenye hotuba aliyotoa baada ya kuapishwa.

Lakini miezi minne baada ya Bw Koome kutoa ahadi hiyo, hajaanzisha mchakato wa kubuni mamlaka hizo.

Sehemu ya 41 ya Sheria ya Huduma ya Kitaifa ya Polisi, 2012 inapendekeza kwamba kubuniwe Mamlaka za Usalama katika kila kaunti nchini.

  • Tags

You can share this post!

Kampuni ya Joho yajitetea kuhusu tenda

Agizo la Gachagua kuhusu pombe halijatekelezwa

T L