• Nairobi
  • Last Updated February 26th, 2024 11:20 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Madai ya wizi wa kura yalishachunguzwa na Mahakama ya Juu

TUSIJE TUKASAHAU: Madai ya wizi wa kura yalishachunguzwa na Mahakama ya Juu

IDARA ya Upelelezi wa Jinai (DCI) imeanzisha uchunguzi wa ripoti kuhusu uwepo wa takwimu mpya ambayo muungano wa Azimio unadai inaonyesha kuwa “ulishinda” katika uchaguzi wa urais Agosti 9, 2022.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa asasi hiyo Mohamed Amin, asasi hiyo inachunguza stakabadhi “zinazosambazwa mitandaoni na kudaiwa kuwa zenye hesabu halisi ya matokeo ya uchaguzi wa urais”.

Bw Amin asije akasahau madai ambayo afisi yake inadai kuchunguza pamoja na kuvurugwa kwa fomu za matokeo ya uchaguzi wa urais yalichunguzwa na Mahakama ya Juu wakati kesi ya kupinga ushindi wa Rais William Ruto mwaka 2022.

Majaji wa mahakama hiyo wakiongozwa na Jaji Mkuu Martha Koome waliamua kuwa stakabadhi hizo zilizowasilishwa na Wakili Judy Soweto zilikuwa ghushi.

Mahakama ya Juu ndiyo taasisi ya kipekee yenye mamlaka ya Kikatiba ya kuchunguza malalamishi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais wala si DCI.

  • Tags

You can share this post!

Musalia Mudavadi atawazwa mlezi wa Baraza la Wazee

Shujaa kuvaana na Fiji, Australia na Japan raga ya Los...

T L