• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Ni vyema Polisi wa Akiba waliotumwa Samburu walipwe marupurupu

TUSIJE TUKASAHAU: Ni vyema Polisi wa Akiba waliotumwa Samburu walipwe marupurupu

KAMISHNA wa Kaunti ya Samburu, Henry Wafula ametangaza kuwa serikali imeajiri jumla ya Polisi 160 wa Akiba (NPR) katika kaunti hiyo ili kusaidia katika udhibiti wa visa vya utovu wa usalama.

Afisa huyo aliongeza kuwa kundi lingine la NPR 200 wakati huu linapokea mafunzo na linatarajiwa kuhitimu baada ya majuma mawili ili kujiunga na wenzao katika mpango wa kusaidiana na polisi wa kawaida kupambana na majangili.

Bw Wafula alisema NPR hao watapewa bunduki na magwanda ya kazi “ili kurahisisha kazi yao”.

Lakini Afisa huyo alikwepa kutaja ikiwa maafisa hao wa NPR watalipwa marupurupu ili kuwatia moyo wanapofanya kazi katika mazingira magumu.

Bw Wafula asije akasahau kuwa mnamo Oktoba 12, 2022 Bunge la Kitaifa lilipitisha hoja iliyopendekeza kuwa maafisa hao wa NPR wawe wakilipwa marupurupu ya hadi Sh14,000 kwa mwezi.

Hoja hiyo ilidhaminiwa na Mbunge wa Mandera ya Mashariki, Abdirahman Mohamed.

Mnamo 2010, hoja sawa na hiyo ilipitishwa katika Bunge la Seneti. Ilidhaminiwa na aliyekuwa Seneta wa Kaunti hiyo Prof John Lonyangapuo.

  • Tags

You can share this post!

Polisi 4 rumande kwa jaribio la kuiba Sh2m

Wafanyakazi wa Mumias wataka msimamizi mpya

T L