• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Polisi 4 rumande kwa jaribio la kuiba Sh2m

Polisi 4 rumande kwa jaribio la kuiba Sh2m

NA RICHARD MUNGUTI

MAAFISA wanne wa polisi wamezuiliwa rumande siku moja polisi wakamilishe uchunguzi wa jaribio la kumnyang’anya kimabavu mmiliki wa duka la kubadilisha pesa za kigeni Sh2,065,000.

Sajini Daniel Wambua Muthini, Koplo Eliud Kipkurui Bor, Konstebo Stanley Gitonga na Konstebo Nicholas Murira watarudishwa kortini kesho (Januari 13) watakaposhtakiwa kwa jaribio la wizi wa mabavu.

Akiamuru wazuiliwe katika kituo cha polisi cha Capitol Hill hakimu mwandamizi Bernard Ochoi alisema washukiwa hao wakiachiliwa watavuruga ushahidi.

“Mlalamishi katika kesi hii anajulikana na washukiwa waliojaribu kumnyang’anya Sh2,065,000 na wakiachiliwa kwa sasa watatatiza uchunguzi,” Bw Ochoi alisema.

Wanne hao walidaiwa walijaribu kumnyang’anya Hassan Omar Abdi, mmiliki wa Afrolite Forex Bureau na mfanyakazi wake Mohammed Omar walioenda kuchukua pesa kutoka Benki ya Absa iliyoko Queensway House.

Bw Ochoi alisema washukiwa hao walijitambua kuwa maafisa wa polisi na kumkamata Abdi na hatimaye wakadai awape hongo lakini akakataa.

“Inabidi polisi wapewe muda kukamilisha uchunguzi,” alisema Bw Ochoi.

  • Tags

You can share this post!

Kioni atabiri Kenya Kwanza itakufa 2027

TUSIJE TUKASAHAU: Ni vyema Polisi wa Akiba waliotumwa...

T L