• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Polisi hawajatimiza ahadi ya kutoa taarifa ya miili iliyotupwa katika mto Yala

TUSIJE TUKASAHAU: Polisi hawajatimiza ahadi ya kutoa taarifa ya miili iliyotupwa katika mto Yala

MNAMO Januari 19, 2022 Msemaji wa Polisi Bruno Shioso aliahidi kutoa taarifa ya kina kuhusu uchunguzi wa tukio ambapo watu walioaminika kuuawa kwingineko ilipatikana katika mto Yala, kaunti ya Siaya.

Alisema kundi la maafisa wa upelelezi wa jinai (DCI) kutoka makao makuu walitumwa Yala ili kushirikiana na wenzao kutoka huko kutegua tendawili hicho ambapo miili ya watu 67 waliotoweka kiajabu mwaka jana, ilipatikana ndani ya magunia.

Kwenye taarifa yake, Bw Bruno aliahidi kutoa taarifa hiyo baada ya majuma mawili kuanzia siku hiyo ili kutanzua kiini cha mauaji hayo na kuwatambua wahusika.

Lakini zaidi ya miezi miwili baadaye, asasi hiyo haijatoa taarifa zozote ilivyoahidi huku habari zikianza kuchipuza kwamba huenda watu hao walikuwa washukiwa wa uhalifu waliouawa na polisi kinyume cha sheria.

Bw Bruno asije akasahau kwamba Wakenya wanasubiri taarifa kuhusu tukio hilo la kuhofisha.

You can share this post!

STEVE ITELA: KWS ibuni mbinu za kisasa kukabili mzozo wa...

Polisi bandia asukumwa jela miezi sita kavu

T L