• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Rais akumbuke IDPs waliotengewa vipande vya ardhi wanahitaji hatimiliki

TUSIJE TUKASAHAU: Rais akumbuke IDPs waliotengewa vipande vya ardhi wanahitaji hatimiliki

RAIS Uhuru Kenyatta na mawaziri wake wanaendesha shughuli ya usambazaji wa jumla ya hatimiliki za ardhi milioni sita katika sehemu mbalimbali nchini.

Akizindua mpango huo mnamo Juni 20, 2022, kiongozi wa taifa, aliwaagiza mawaziri kushirikiana na makamishna katika kaunti zote 47 nchini kuhakikisha kuwa shughuli hiyo inakamilishwa kabla ya uchaguzi mkuu Agosti 9.

Lakini serikali isije ikasahau kuwa, waathiriwa wa ghasia za kisiasa za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 (IDPs) ambao iliwapa ardhi mbadala katika sehemu za Laikipia, Nyandarua, Nakuru, Uasin Gishu na Trans Nzoia, hawajapewa hatimiliki za ardhi ilizowapa kati ya 2013 na 2014.

Katibu wa Shirika la Kitaifa la IDPs, Raphael Eyanai analalamika kuwa ardhi ambazo walipewa na serikali hii ya Jubilee,kama fidia, vile vile hazijafanyiwa usoroveya inavyohitajika kisheria.

Sasa anamtaka Rais Kenyatta kuamuru IDPs wote wapewe stakabadhi hizo muhimu kabla ya Agosti 9, ili waweze kutumia mashamba hayo kwa shughuli halali za kuwaletea mapato.

  • Tags

You can share this post!

Sterling kirasmi aingia Chelsea

Matusi ya viongozi yaaibisha serikali

T L