• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
TUSIJE TUKASAHAU: Tungali tuna kibarua kutokomeza ukeketaji

TUSIJE TUKASAHAU: Tungali tuna kibarua kutokomeza ukeketaji

MNAMO Jumatano wiki hii watu saba walikamatwa katika kaunti ya Nyeri baada ya kuhusishwa na ukeketaji wa wasichana wanane wenye umri mdogo.

Visa vya ukeketaji wa wasichana pia vimekuwa vikiripotiwa katika kaunti za Narok, Kajiado, Nyamira, Migori, Wajir miongoni mwa maeneo mengine.

Hii ni licha ya kwamba utamaduni huu ulipigwa marufuku kuanzia mwaka wa 2011 kupitia sheria iliyopitishwa bungeni.

Sheria hiyo imeweka adhabu ya faini isiyopungua Sh50,000 kifungo cha miaka mitatu gerezani au adhabu zote mbili kwa watakaopatikana na kosa la kuendeleza ukeketaji.

Tusije tukasahau kwamba, visa hivi vinaendelea kuripotiwa, haswa katika eneo la Kati mwa Kenya ambako vilikuwa vimetokomezwa, ilhali Waziri wa Utumishi wa Umma Margaret Kobia aliahidi kuvitokomeza kufikia mwaka huu wa 2022.

Profesa Kobia alitoa ahadi hii mnamo 2019 wakati ambapo alifichua kupungua kwa visa hivyo nchini kutoka asilimia 27 mnamo 2013 hadi asilimia 18 mwaka huo.

  • Tags

You can share this post!

Mudavadi kuwa tu waziri katika serikali ya Ruto

NCIC yapiga marufuku baadhi ya maneno na msamiati katika...

T L