• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
WANGU KANURI: Rais ahakikishe wanafunzi kote nchini wanapata thamani ya mtaala wa CBC

WANGU KANURI: Rais ahakikishe wanafunzi kote nchini wanapata thamani ya mtaala wa CBC

NA WANGU KANURI

JUMATANO iliyopita, Rais William Ruto, akiongea na wanahabari katika Ikulu ya Nairobi, alikiri kuwa mtaala mpya wa elimu wa CBC ni mzuri na utasaidia sana wanafunzi kwani matokeo yake yana faida tele.

Rais alisema licha ya kuwa CBC ni nzuri, serikali iliharakisha katika utekelezaji wa mtaala huo kabla ya kuweka mipango thabiti.

Alisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wazazi walipendekeza wanafunzi wa Gredi ya Saba kuwa karibu na wazazi wao kwa sababu wangali wadogo mno wa kusomea katika shule za bweni zilizoko mbali na nyumbani.

Kutokana na maoni hayo ya wazazi wengi, Jopokazi lililochaguliwa na rais kushughulikia utekelezaji na marekebisho katika mtaala wa CBC, lilipendekeza wanafunzi wa Gredi ya 7 waendelee kusomea katika shule za msingi walikokuwa.

Hata hivyo, kuna changamoto ambazo zinastahili kuangaziwa zaidi kwani masomo ya Gredi ya 7 ni ya sekondari na yanahitaji vifaa zaidi kama vile maabara, maktaba, karakana za masomo ya sanaa miongoni mwa mahitaji mengine.

Kwa kuwa vifaa hivi havipo pamoja na walimu wa kutosha wa kufunza Gredi ya 7-9, rais hana budi kubeba mzigo huo ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wa Gredi ya 7 hadi 9 wanapata elimu bora inayokusudiwa na mtaala wenyewe.

Kuna hatari ya masomo ya sekondari ya chini kuvurugika na kukosa kuafikia malengo ikiwa mikakati ifaayo haitawekwa.

Rais anahitaji kuchukua jukumu hilo mwenyewe ili kuokoa maisha ya wanafunzi zaidi ya 2.5 milioni watakaojiunga na Gredi ya 7.

Ikiwa, kwa mfano serikali haitaajiri walimu 30,000 kama ilivyoahidi, hilo litakuwa ni kosa la kwanza kwani walimu walioko katika shule za msingi sasa hivi hawatoshi na ni wachache mno walio na elimu inayohitajika kufunza sekondari ya chini.

  • Tags

You can share this post!

Ruto alivyofuta mawaziri wasaidizi wa Uhuru kimya kimya

CHARLES WASONGA: Ruto ajizatiti kukomesha ufisadi na...

T L