• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
AFCON: Uga wa Olembe waidhinishwa kutumika kwa ajili ya mechi za nusu-fainali na fainali

AFCON: Uga wa Olembe waidhinishwa kutumika kwa ajili ya mechi za nusu-fainali na fainali

Na MASHIRIKA

UWANJA wa Olembe jijini Yaounde, Cameroon umeidhinishwa kutumika kuandalia mechi za nusu-fainali na fainali ya Kombe la Afrika (AFCON) mwaka huu, siku chache baada ya mkanyagano wa mashabiki kutokea nje ya uga huo.

Watu wanane waliaga dunia na 38 wengine kuumia wenyeji Cameroon walipokuwa wakivaana na Comoros kwenye hatua ya 16-bora mnamo Januari 24, 2022.

Tangazo la kuidhinisha uwanja wa Olembe kutumika lilitolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) baada ya kupokea ripoti kuhusiana na tukio hilo la mkanyagano.

Kwa mujibu wa CAF, ajali iliyoshuhudiwa nje ya uwanja wa Olembe haukutokana na ubovu wa uga wenyewe bali msukumano wa maelfu ya mashabiki waliokuwa wakiwania fursa ya kuingia ndani ya uga huo unaoruhusiwa kubeba asilimia 80 pekee ya mashabiki kwa sababu ya janga la corona.

Mvulana mwenye umri wa miaka minane alikuwa miongoni mwa walioangamia kwenye mkanyagano huo.

Uga wa Olembe ulio na uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ulitarajiwa kutumiwa kuandalia mchuano wa robo-fainali kati ya Misri na Morocco mnamo Januari 30 ila gozi hilo likahamishiwa uwanjani Ahmadou Ahidjo.

Uwanja wa Olembe sasa utatumiwa kwa ajili ya nusu-fainali kati ya Misri na wenyeji Cameroon mnamo Februari 3, 2022 na fainali itakayotandazwa Februari 6, 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Simiu na Jeruto moto wa kuotea mbali mbio za nyika za...

Joy Mwende, chipukizi anayepepea katika ushonaji na uigizaji

T L