• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Argentina wacharaza Venezuela katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia

Argentina wacharaza Venezuela katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia

Na MASHIRIKA

TIMU ya taifa ya Argentina ilipachika wavuni mabao mawili chini ya dakika tatu za kipindi cha pili na kukomoa Venezuela 3-0 jijini Buenos Aires kwenye mchuano wa kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Dunia nchini Qatar.

Mabingwa hao wa Copa America ambao wametawazwa wafalme wa Kombe la Dunia mara mbili, sasa wataungana na Brazil, Ecuador na Uruguay nchini Qatar kwa Kombe la Dunia kati ya Novemba na Disemba 2022. Peru, Colombia na Chile wangali katika vita vya kupigania fursa ya kumaliza kampeni za mataifa 10 kutoka Amerika Kusini katika nafasi ya tano ili kufuzu kwa mchujo wa mwisho dhidi ya mpinzani kutoka bara Asia.

Venezuela ndicho kikosi cha pekee kati ya 10 kutoka Amerika Kusini kutowahi kufuzu kwa Kombe la Dunia. Kichapo kutoka kwa Argentina kilikuwa chao cha 10 kutokana na mechi 12 zilizopita.

Argentina waliofunga mabao yao kupitia Nicolas Gonzalez, Angel Di Maria na Lionel Messi, sasa hawajapoteza mechi yoyote kati ya 30 zilizopita chini ya kocha Lionel Scaloni aliyetwaa mikoba yao mnamo Julai 2019.

Kikosi hicho kilichokosa huduma za wanasoka wanne waliopigwa marufuku kwa kukiuka kanuni za Covid-19 mnamo Septemba 2021, hakijawahi kupigwa na Venezuela mbele ya mashabiki wa nyumbani kutokana na mechi nane mfululizo.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kuria aagizwa kufika mbele ya kamati ya IEBC

Mgombea udiwani wadi ya Kiuu ajipambanua kama kiongozi wa...

T L