• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 8:22 PM
Ariel Okall arejea Uganda kuchezea KIU Titans baada ya Oman kusitisha michezo

Ariel Okall arejea Uganda kuchezea KIU Titans baada ya Oman kusitisha michezo

Na GEOFFREY ANENE

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya mpira wa vikapu ya wanaume ya Kenya, Ariel Okall amejiunga na timu ya Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala maarufu kama KIU Titans nchini Uganda.

Okall, ambaye alikuwa katika timu ya Kenya Morans iliyofuzu mwezi Februari kushiriki Kombe la Bara Afrika (AfroBasket) litakalofanyika baadaye mwaka huu nchini Rwanda, amejiunga na KIU Titans kutoka nchini Oman.

Aliwahi kuchezea klabu ya Falcons ya Chuo Kikuu cha Makerere mwaka 2015 kabla ya kuendeleza taaluma yake nchini Tanzania, Ushelisheli, Oman, Kenya na Algeria na kurudi Oman mwezi Februari. Hata hivyo, taifa hilo la Uarabuni lilisitisha michezo baada ya Machi 30 kutokana na janga la corona. Okall aliamua kurejea nchini zaidi ya wiki moja iliyopita.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliaminika kuwa mbioni kujiunga na City Oilers ambao wameshinda Ligi Kuu ya Uganda mara saba mfululizo. Hata hivyo, ripoti nchini Uganda zimethibitisha kuwa amesaini kandarasi fupi na KIU Titans.

  • Tags

You can share this post!

Man-City wapiga Palace 2-0 na kunusia ubingwa wa EPL

JAMVI: Mtihani wa IEBC 2022 vigogo wa siasa nchini...