• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 12:18 PM
Bandari kuwakosa chipukizi wawili wenye majeraha mabaya

Bandari kuwakosa chipukizi wawili wenye majeraha mabaya

KIUNGO mshambuliaji wa Bandari FC, Mohamed Abeid hataweza kuichezea timu yake hiyo kwa kipindi cha miezi sita ama saba baada ya kuumia na kuhitaji kufanyiwa upasuaji utakaomweka nje kwa kipindi hicho.

Kocha wa Bandari FC Anthony Kimani amesema Abeid almaarufu Mudiga alipata jeraha la goti katika mojawapo ya mechi zao za kujipima nguvu na alipofanyiwa uchunguzi zaidi ilionekana ameumia zaidi na atahitajika kufanyiwa upasuaji utakaomuweka nje kwa kipindi kirefu.

“Kijana mdogo ambaye alipata nafasi ya kujiunga na sisi na labda angelipata nafasi kubwa sana ya kucheza msimu unaokuja kwa sababu ya uwezo wake lakini kutokana na kufanyiwa matibabu, hatutakuwa naye kwa miezi sita ama saba,” akasema Kimani.

Mkufunzi huyo alikuwa akiongea baada ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya klabu ya Mwatate United kutoka Kaunti ya Taita Taveta iliyofanyika uwanja wa Mbaraki Sports Club na kuibuka washindi wa bao 1-0.

Kimani alisema mchezaji mwingine ambaye watamkosa ni Omar Somoebwana ambaye amevunjika mfupa kwenye mkono wake na atahitaji matibabu yatakayochukua muda wa kipindi cha miezi miwili.

Kuhusiana na mchezo wao na Mwatate United inayoshiriki Supaligi ya Taifa (NSL), Kimani alisema wamepata msukumo na mazoezi mazuri kutoka kwa wapinzani wao hao ambao anasema hawakuwa rahisi.

“Nimefurahi kwa kuwa tumewapa wachezaji wetu wengi nafasi ya kucheza mechi ambayo ilikuwa na uzito na kasi tunayotarajia kupambana nayo wakati tutakapoanza kucheza mechi zetu za msimu ujao za Ligi Kuu ya Kenya,” akasema mkufunzi huyo.

  • Tags

You can share this post!

Hasara lori la unga wa Sh2.6 milioni likipata ajali karibu...

Mvua ya unga yanyeshea raia

T L