• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 7:50 AM
Barca nje ya 16-bora taji la UEFA

Barca nje ya 16-bora taji la UEFA

MUNICH, Ujerumani

Na MASHIRIKA

BARCELONA imepigwa na butwaa baada ya kubanduliwa kwenye kinyang’anyiro cha Klabu Bingwa barani Ulaya (UEFA) kwa mara ya kwanza katika muda wa miaka 17 iliyopita.

Hii ni baada ya kupokezwa kichapo cha 3-0 a Bayern Munich ya Ujerumani kwenye mechi iliyochezwa Jumatatu usiku na hivyo kumaliza katika nafasi ya tatu. Benfica ya Ureno ilifuzu kwa kuibuka nambari mbili kundini.Sasa Barcelona watacheza katika mchujo wa mechi za Europa League ambayo ni ya daraja la chini.A

kizungumza na waandishi wa habari, kiungo Sergio Busquets alisema: ‘Tumefedheheshwa mno na matokeo haya ambayo yametuweka katika hali ngumu. Tutajilaumu wenyewe kwa yaliyotokea.’Mara ya mwisho Barcelona kukosa kushiriki katika michuano ya Klabu Bingwa ilikuwa msimu wa 2003-04 baada ya kubanduliwa na Celtic.

Nyumbani katika Ligi kuu ya Uhispania (La Liga) Barcelona wanakamati nafasi ya saba na majuzi wamemfuta kazi Ronald Koeman na kumpa jukumu hilo aliyekuwa nahodha wao Xavi.Kichapo kutoka kwa Bayern Munich kimekuja pia wakati klabu hii inakabiliwa na matatizo mengi ya kifedha yaliyosababisha kuondoka kwa staa Lionel Messi na kujiunga na Paris St-Germain kama mchezaji huru.

Kubaduliwa kwao kulitokana na ushindi wa Benfica wa 2-0 dhidi ya Dynamo Kyiv. Thomas Muller alifunga bao la kwanza baada ya kuandaliwa na Robert Lewandowski, kabla ya Leroy Sane kuongeza la pili kutokana na kombora la umbali wa yadi 30.

Jamal Musiala aliongeza bao la tatu katika kipindi cha pili baada ya kuunganisha mpira wa Alphonso Davies.Droo ya mechi za 16 bora itafanyika Jumatatu mjini Nyon, Uswizi.

You can share this post!

Arsenal matumaini tele itajifufua ikipepetana na...

Helikopta kutumika Mama Lucy mwakani kutoa huduma- NMS

T L