• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Beki Marcelo kuondoka Bernabeu akiwa mchezaji anayejivunia idadi kubwa zaidi ya mataji kambini mwa Real Madrid

Beki Marcelo kuondoka Bernabeu akiwa mchezaji anayejivunia idadi kubwa zaidi ya mataji kambini mwa Real Madrid

Na MASHIRIKA

MIAKA 15 baada ya kutua Real Madrid akilenga kuwa mrithi wa beki Roberto Carlos, Marcelo ataagana rasmi na miamba hao wa Uhispania na bara Ulaya akiwa mchezaji anayejivunia idadi kubwa zaidi ya mataji katika historia ya klabu hiyo.

Marcelo, 34, alimpiku Paco Gento – ambaye alishindia Real mataji sita ya European Cup katika miaka ya 1950 na 1960 – aliponyanyua taji lake la sita la La Liga mnamo Aprili 2022 na hivyo kufikisha jumla ya mataji yake kuwa 25 akivalia jezi za Real.

Ushindi wa 1-0 uliosajiliwa na Real dhidi ya Liverpool mnamo Mei 28, 2022 jijini Paris, Ufaransa ulimzolea Marcelo taji lake la tano katika soka ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

“Mchuano huo ulikuwa wangu wa mwisho kambini mwa Real. Kuagana na kikosi hicho ukijivunia taji la UEFA ni tija na fahari tele,” akasema Marcelo aliyeshuhudia waajiri wake wakitwaa taji la 14 la UEFA.

Marcelo alijiunga na Real akiwa na umri wa miaka 19 baada ya kuagana rasmi na Fluminense mnamo Januari 2007. Nyota huyo raia wa Brazil amekuwa tegemeo la Real kama beki wa kushoto kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Kusajiliwa kwake kambini mwa Real kulichochewa na haja ya kujazwa kwa pengo la Roberto Carlos aliyeyoyomea Uturuki kuvalia jezi za Fenerbahce.

Tangu wakati huo, amechezea Real mara 500 na akashindia kikosi hicho mataji kadhaa ya La Liga na UEFA, manne ya Kombe la Dunia, matatu ya European Super Cups, matano ya Spanish Super Cups na mawili ya Copa del Rey. Alichezea Real mara 18 katika mashindano yote ya msimu huu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Lewandowski asema haoni uwezekano wa kuendelea kuwa...

Beki Ben White ajiondoa kambini mwa Uingereza kwa sababu ya...

T L