• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 1:13 PM
Brazil kuvaana na Mexico katika nusu-fainali za Olimpiki baada ya kuichapa Misri

Brazil kuvaana na Mexico katika nusu-fainali za Olimpiki baada ya kuichapa Misri

Na MASHIRIKA

MABINGWA watetezi Brazil walifuzu kwa nusu-fainali za soka ya Olimpiki mnamo Julai 31, 2021 baada ya kuwapokeza Misri kichapo cha 1-0 jijini Yokohama, Japan.

Brazil walifungiwa bao la pekee na la ushindi katika gozi hilo kupitia Matheus Cunha.

Ushindi wa Brazil uliwakatia tiketi ya nusu-fainali ambayo sasa itawakutanisha na Mexico waliotwaa dhahabu mnamo 2012 jijini London, Uingereza.

Mexico waliwakung’uta Korea Kusini 6-3 kwenye robo-fainali nyingine mnamo Julai 31, 2021.

Martin aliwaweka Mexico kifua mbele kunako dakika ya 12 kabla ya Lee Dong-gyeong kusawazisha mambo dakika nane baadaye.

Romo alirejesha Mexico uongozini katika dakika ya 29 baada ya kuandaliwa pasi na Vega.

Cordova alifungia Mexico goli la pili kupitia penalti baada ya Uriel Antuna kuchezewa visivyo ndani ya kijisanduku.

Ingawa Lee aliwarejesha Korea Kusini mchezoni, makali yao yalizimwa na Martin kabla ya Cordova, Diego Lainez na Eduardo Aguirre kufunga mabao mengine.

Hwang Ui-jo alifungia Korea Kusini goli la tatu.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Uhispania wakomoa Ivory Coast na kufuzu kwa nusu-fainali za...

TAHARIRI: Uteuzi na mbinu mbovu tatizo letu