• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Chepng’etich atwaa taji Nagoya Marathon, avuna Sh28.5m

Chepng’etich atwaa taji Nagoya Marathon, avuna Sh28.5m

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA Ruth Chepng’etich ameibuka malkia wa Nagoya Marathon kwa rekodi mpya ya mbio hizo za kinadada ya saa 2:17:18 nchini Japan, Jumapili.

Bingwa huyo wa dunia, ambaye anajivunia muda wake bora wa 2:17:08 kutoka Dubai Marathon 2019, alikuwa amepigiwa upatu kutawala mbio hizo zenye tuzo kubwa kabisa duniani ya mshindi ya Sh28.5 milioni.

Alitimiza ndoto hiyo kwa kuwabwaga wapinzani wake wa karibu Lonah Chemtai Salpeter (Israel) na Yuka Ando (Japan) mtawalia.

Bingwa wa Chicago Marathon 2021 Chepngetich alikata utepe katika eneo la Vantelin Dome Nagoya zaidi ya dakika moja mbele ya mzawa wa Kenya, Salpeter (2:18:45) naye Ando alikamilisha kwa 2:22:22.

Vita vya kunyakua taji vilisalia kuwa kati ya Chepng’etich na Salpeter baada ya kilomita ya 30. Hata hivyo, Chepng’etich alimuacha Salpeter zikisalia kilomita nane.

Matokeo (10-bora):

1. Ruth Chepngetich (Kenya) saa 2:17:18

2. Lonah Chemptai Salpeter (Israel) 2:18:45

3. Yuka Ando (Japan) 2:22:22

4. Ai Hosoda (Japan) 2:24:26

5. Yuka Suzuki (Japan) 2:25:02

6. Eloise Wellings (Astralia) 2:25:10

7. Ikumi Fukura (Japan) 2:25:15

8. Kotona Ota (Japan) 2:25:56

9. Kanako Takemoto (Japan) 2:26:23

10. Chiharu Ikeda (Japan) 2:26:50

  • Tags

You can share this post!

Bayern na Hoffenheim nguvu sawa katika Bundesliga

KIGODA CHA PWANI: Hofu wanawake wakikosa kujitegemea...

T L