• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 9:50 AM
Chepng’etich kivutio Istanbul Half Marathon nchini Uturuki

Chepng’etich kivutio Istanbul Half Marathon nchini Uturuki

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA mara tatu wa N Kolay Istanbul Half Marathon, Ruth Chepng’etich atakuwa kivutio katika makala ya 2023 yatakayofanyika nchini Uturuki mnamo Aprili 30.

Chepng’etich ametiwa katika orodha ya watimkaji 12,060 kutoka mataifa 60 watakaoshiriki mbio hizo.

Afisa huyo kutoka Idara ya Magereza alinyakua mataji ya Istanbul Half Marathon mwaka 2017 kwa saa 1:06:19, mwaka 2019 kwa 1:05:30 iliyokuwa rekodi ya Istanbul Half wakati huo kabla ya kuweka rekodi mpya ya kilomita 21 ya 1:04:02 mwaka 2021 iliyokuwa pia rekodi ya dunia.

Amezoa matokeo mazuri Uturuki ikiwemo pia kutawala mbio za kilomita 42 mjini Istanbul mwaka 2017 na 2018.

Bingwa huyo wa marathon za Chicago 2021 na 2022 na dunia 2019 atakutana na Mturuki Gunen aliye na muda bora katika 21km (1:10:27), miongoni mwa wengine.

Mshindi wa Barcelona Half Marathon Charles Kipkurui Langat ni mmoja wa majina makubwa katika kitengo cha wanaume. Anajivunia muda bora katika 21km wa dakika 58:53.

  • Tags

You can share this post!

FENCING: Alexandra Ndolo ajizolea sifa kwa kupigana kwa...

Markstam Orwa asema bidii inaweza kumfikisha kwa viwango...

T L