• Nairobi
  • Last Updated April 26th, 2024 7:00 PM
Chepng’etich kuvizia rekodi ya dunia ya 1500m Monaco Diamond League

Chepng’etich kuvizia rekodi ya dunia ya 1500m Monaco Diamond League

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Faith Chepng’etich Kipyegon huenda akatimiza ndoto yake ya kuwa mshikilizi wa rekodi ya dunia ya mbio za mita 1,500 atakapotimka kwenye duru ya Diamond League ya Monaco mnamo Julai 21.

Bingwa huyo wa Jumuiya ya Madola, Olimpiki na dunia wa mbio hizo za mizunguko minne alikosa rekodi ya dunia ya Muethiopia Genzebe Dibaba ya dakika 3:50.07, baada ya kufyatuka 3:50.37 kwenye duru hiyo ya Monaco maarufu kama Herculis mwaka 2022.

Aliandikisha muda huo wiki tatu baada ya kutwaa taji lake la pili la dunia kwa dakika 3:52.96 mjini Eugene, Amerika.

Chepngetich alikamilisha msimu huo kwa kushinda fainali yake ya tatu ya Diamond League mjini Zurich, Uswisi.

Rekodi nne za dunia zilizowekwa Monaco zingali imara. Kuna rekodi ya 1500m ya 3:50.07 iliyowekwa na Dibaba mnamo Julai 17, 2015.

Mholanzi mwenye asili ya Ethiopia Sifan Hassan anashikilia rekodi ya dunia ya maili moja ya 4:12.33 aliyoweka Julai 12, 2019.

Mkenya Beatrice Chepkoech alishinda 3,000m kuruka viunzi na maji kwa rekodi ya dunia ya dakika 8:44.32 mnamo Julai 20, 2018.

Rekodi ya mwisho kuwekwa Monaco ni ya 5,000m wanaume ambapo Mganda Joshua Cheptegei alitimka 12:35.36 mnamo Agosti 14, 2020.

Inaaminika Chepng’etich atatafuta kasi ya juu mjini Herculis, Monaco hapo Julai 21 akijiandaa kwa Riadha za Dunia zitakazofanyika mjini Budapest, Hungary mnamo Agosti 19-27.

Alifungua msimu kwa kushinda duru ya kwanza ya Diamond League mjini Doha, Qatar kwa dakika 3:58.57 mnamo Mei 5.

Bingwa wa Diamond League, Olimpiki na dunia mbio za 800m Emmanuel Korir kutoka Kenya pia atakimbia mjini Herculis kabla ya Riadha za Dunia.

  • Tags

You can share this post!

Ruto amteua mke wa Chebukati awe mwenyekiti wa CRA

Mbunge Alice Ng’ang’a atoa basari, aahidi...

T L