• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 10:55 AM
Cheruiyot ang’aria wapinzani mita 800 Riadha za AK

Cheruiyot ang’aria wapinzani mita 800 Riadha za AK

Na GEOFFREY ANENE

BINGWA wa dunia mbio za mita 1,500, Timothy Cheruiyot ni mmoja wa wanariadha waliong’ara katika siku ya mwisho ya duru ya mashindano ya Shirikisho la Riadha Kenya (AK) uwanani Moi mjini Kisumu, Jumamosi.

Nyota huyo kutoka Idara ya Magereza alibeba taji la mbio za mita 800. Bingwa wa Barcelona Half Marathon Sandrafelis Chebet (mita 10,000), Elijah Mathew (mita 100), Dominic Ndigiti (kutembea haraka mita 10,000), Sylvia Kemboi (kutembea haraka mita 10,000) na Vincent Mutai (mbio za mita 10,000).

Wengine waliovuna ushindi ni Millicent Ndoro (mita 100), Linda Kageha (mita 400), Wycliffe Kinyamal (mita 400) na Mercy Chebet (mita 200). Ushindi wa Chebet ulikuwa wa pili wikendi hii baada ya kunyakua taji la mbio za mita 10,000 kwa dakika 34:32.4 Ijumaa. Mnamo Jumamosi, Chebet alikamilisha mizunguko 12 na nusu kwa dakika 15:34.0.

Irene Kamais aliridhika na nafasi ya pili kwa dakika 15:50.3 naye Miriam Cherop akafunga tatu-bora 53:53.2. “Lengo langu katika duru ya Kisumu ilikuwa kumaliza wa kwanza. Nafurahi sana kuwa nimetimiza lengo hilo katika vitengo vyote viwili,” alisema.

Cheruiyot, ambaye alishinda medali ya fedha mita 1,500 kwenye Olimpiki 2020 nchini Japan, alikamilisha mizunguko yake miwili kwa dakika 1:46.8. Bingwa huyo wa Diamond League mbio za mita 1,500 mwaka 2017, 2018, 2019, 2021 alifuatiwa kwa karibu na Macdonal Kipruto (1:47.2) na Norbert Kolombos (1.47.1) mtawalia.

Bingwa wa Afrika Under-20 Ndigiti alitwaa taji la kutembea kwa haraka mita 10,000 alipoandikisha dakika 46:13.6. Mshindi wa medali ya shaba ya Kip Keino Classic 2020 Eric Sikuku alikamata nafasi ya pili (47:33.3) naye Dominic Mwendwa akawa wa tatu (52:14.6).

You can share this post!

Msusi atoboa siri

Impala yanining’inia pabaya Kenya Cup baada ya kichapo

T L