• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Compel FC yaongoza ligi ya Zoni A Daraja la Pili

Compel FC yaongoza ligi ya Zoni A Daraja la Pili

NA JOHN KIMWERE

TIMU ya Compel FC imerukia uongozi wa mechi za Zoni A Kanda ya Magharibi Ligi ya Taifa Daraja la Pili baada ya kuzaba Westkenya Allstars kwa mabao 5-0 wikendi.

Kocha wake, George Mutiba ameshukuru vijana wake kwa kujituma na kutua kileleni mwa jedwali la ngarambe hiyo.

“Tumepania kuendeleza mtindo wa kujituma kiume kupigania tiketi ya kushiriki mini-ligi ili angalau tupanda ngazi msimu ujao,” kocha wa Compel alisema.

Nayo Butali Sugar ilizoa alama tatu baada ya kuzaba Youngstar mabao 2-0 huku Malaba Giants ikinyukwa mabao 2-1 na Eshimambo FC.

Kwenye mfululizo wa matokeo hayo, kwa mara nyingine, Opet FC iliagana sare tasa dhidi ya Bungoma Stars FC.

Kocha mkuu wa Opet FC, Joseph Murno Opochi anasema kuwa lazima wajitahidi kiume watakapokabili wapinzani wao ili kutwaa tiketi ya kushiriki mini-ligi msimu huu.

“Ninashukuru wachezaji wangu kwa kuzingatia hawapotezi patashika hiyo ingawa hatukutimiza azma yetu ya kubeba alama tatu muhimu,” kocha wa Opet alisema.

Alitoa wito kwa wachezaji wake kamwe wasilaze damu kwenye mechi zijazo.

Hata hivyo alidokeza kuwa timu zinazojitoa kwenye ligi zinawafanya wapokonywe pointi muhimu. Kutokana na matokeo hayo, Compel FC inaongoza kwa alama 44 kutokana na mechi 22.

Nayo Bungoma Stars inashikilia nafasi ya pili kwa alama 37, sawa na Opet FC baada ya kushiriki mechi 20 kila moja.

  • Tags

You can share this post!

12 wakwama katika jengo liliporomoka Murang’a  

Aston Villa waajiri Monchi kuwa rais wao wa masuala ya soka

T L