• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Covid-19 yavuruga maandalizi ya timu ya taifa ya Zimbabwe kwa minajili ya fainali za CHAN 2021

Covid-19 yavuruga maandalizi ya timu ya taifa ya Zimbabwe kwa minajili ya fainali za CHAN 2021

Na MASHIRIKA

MAANDALIZI ya timu ya taifa ya Zimbabwe kwa minajili ya kampeni zijazo za Kombe la Afrika kwa wanasoka wa klabu za nyumbani (CHAN) 2021 nchini Cameroon sasa yamevurugika baada ya wanasoka tisa kuugua Covid-19 wakiwa kambini.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Zimbabwe (Zifa), jumla ya wanasoka tisa walipatikana na virusi vya corona baada ya kikosi kizima cha wanasoka 23 na maafisa wa benchi ya kiufundi kufanyiwa vipimo vya afya baada ya sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya.

“Waathiriwa wote ambao kwa sasa wameshauriwa kujitenga kwa siku 14, wamearifiwa kueleza familia zao kuhusu hali zao pamoja na wale waliotangamana nao kwa karibu msimu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya,” ikasema sehemu ya taarifa ya Zifa kwa kufichua kwamba kambi ya timu ya taifa ya Zimbabwe sasa imevunjwa na vipindi vya mazoezi kusitishwa.

Tukio hilo ni pigo kubwa kwa kikosi cha Zimbabwe kinachojiandaa kwa mapambano ya CHAN ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi mnamo Januari 16, 2020 nchini Cameroon.

Zifa imethibitisha pia kufutiliwa mbali kwa mechi mbili za kirafiki zilizokuwa ziwakutanishe na Kenya na Congo mwezi huu wa Januari 2021.

“Covid-19 imevuruga mipango yote ya usafiri na kwa sasa itakuwa vigumu kwa kikosi kushiriki mechi mbili za kirafiki zilizokuwa zimepangwa,” akasema meneja wa timu ya Zimbabwe, Wellington Mupandare.

Wakati uo huo, Rwanda wamefichua mipango ya kujiondoa kwenye fainali za CHAN mwaka huu kwa madai kwamba corona imefanya bajeti yao kwa minajili ya kivumbi hicho kuwa juu zaidi na huenda isiwezekane kwa ufadhili kupatikana kwa wakati.

Zimbabwe wamo katika Kundi A la kipute hicho cha CHAN kwa pamoja na Burkina Faso, Mali na wenyeji Cameroon. Kwa mujibu wa ratiba, Zimabwe almaarufu The Warriors wanatarajiwa kufungua rasmi kampeni za kipute hicho dhidi ya Cameroon mnamo Januari 16 na wanatarajiwa kuondoka jijini Harare mnamo Januari 11, 2021 kuelekea jijini Yaounde, Cameroon.

  • Tags

You can share this post!

Dereva wa magari ya langalanga Lewis Hamilton sasa atakuwa...

Wazazi Thika wafurika madukani kuwanunulia watoto wao sare,...