• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
eki Nuno Tavares atua London kukamilisha uhamisho wake hadi Arsenal

eki Nuno Tavares atua London kukamilisha uhamisho wake hadi Arsenal

Na MASHIRIKA

BEKI Nuno Tavares ametua jijini London, Uingereza kukamilisha uhamisho wake kutoka Benfica hadi Arsenal kwa kima cha Sh1 bilioni.

Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kuhudumu kambini mwa Arsenal hadi mwisho wa Juni 2026.

Anatazamiwa kumpiga jeki difenda Kieran Tierney ambaye nafasi yake imekuwa ikitwaliwa na Bukayo Saka au Granit Xhaka kila anapolazimika kukosa mechi.

Tavares alionekana na wakala wake Rafael Santos nje ya makao makuu ya Arsenal mnamo Julai 3, 2021 wakipiga picha kabla ya kukutana na maafisa wa kikosi hicho uwanjani Emirates.

Beki huyo anakuwa sajili wa kwanza wa Arsenal wanaolenga kujisuka upya chini ya kocha Mikel Arteta muhula huu.

“Ni rasmi kwamba Tavares sasa ni mali ya Arsenal. Ametia saini mkataba wa muda mrefu hadi Juni 2026. Atakuwa akibadilishana zamu na Tierney ambaye ni beki mahiri raia wa Scotland,” ikasema sehemu ya taarifa ya Arsenal.

Tavares aliwajibishwa na Benfica katika mechi 25 za mashindano yote mnamo 2020-21 na akachangia mabao matatu.

Nahodha wa Anderlechet ya Ubelgiji, Albert Sambi, ni mwanasoka mwingine anayetarajiwa kuingia katika sajili rasmi ya Arsenal kufikia Julai 6, 2021 ili awe kizibo cha kiungo Matteo Guendouzi anayehusishwa pakubwa na Olympique Marseille ya Ufaransa.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

ODM yapuuza madai ya kupoteza ufuasi Pwani

Wolves wamsajili mshambuliaji Francisco Trincao kutoka...