• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 6:26 PM
EPL: Everton walaza Leicester na kujiondoa katika hatari ya kuteremshwa ngazi

EPL: Everton walaza Leicester na kujiondoa katika hatari ya kuteremshwa ngazi

Na MASHIRIKA

EVERTON walijiondoa katika hatari ya kuteremshwa ngazi katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mwishoni mwa msimu huu baada ya kupokeza Leicester City kichapo cha 2-1 mnamo Jumapili ugani King Power.

Mabao kutoka kwa Vitaliy Mykolenko na Mason Holgate yalivunia Everton wanaonolewa na kocha Frank Lampard ushindi wao wa tatu kutokana na mechi tano na hivyo kuweka hai matumaini ya kusalia ligini msimu ujao kadri wanavyojiandaa kwa mechi nne zaidi za muhula huu.

Mykolenko alifungulia Everton ukurasa wa mabao katika dakika ya sita baada ya kushirikiana na Alex Iwobi kabla ya Patson Daka kukamilisha krosi ya Yerry Mina na kusawazishia Leicester dakika tano baadaye.

Holgate alipachika wavuni bao la ushindi kwa upande wa Everton katika dakika ya 30 baada ya kumwacha hoi kipa Kasper Schmeichel aliyetatizwa pakubwa na fowadi Richarlison Andrade.

Ushindi huo ulikweza Everton hadi nafasi ya 16 kwa alama 35, moja zaidi kuliko Burnley na Leeds United waliopepetwa 2-1 na Arsenal.

Kushindwa kwa Leicester kuliendeleza rekodi yao ya kutoshinda mechi tano zilizopita za EPL na sasa wanashikilia nafasi ya 14 jedwalini kwa alama 42, moja nyuma ya Aston Villa, Brentford na Newcastle United waliopokezwa kichapo kinono cha 5-0 kutoka kwa Newcastle United.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Chogo alenga kufikia kiwango cha nyota Cristiano Ronaldo wa...

Shiney apiga abautani akiweka zingatio kwa muziki wa Injili

T L