• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Equator Rally kushuhudia kivumbi kikali magari saba ya kisasa ya R5 yakishiriki

Equator Rally kushuhudia kivumbi kikali magari saba ya kisasa ya R5 yakishiriki

Na GEOFFREY ANENE

Madereva wanaamini kuingia kwa magari ya R5 katika duru ya Mbio za Magari za Afrika (ARC) ya Equator Rally ni dalili kuwa mambo mazuri yako njiani.

Bingwa mwelekezi wa daraja ya kwanza ya Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) Victor Okundi anasema,”Hii inaonyesha jinsi Bara Afrika imeimarika katika mchezo huu! Madereva wamewekeza pakubwa katika mashine za kisasa wanazoendesha ishara kuwa wanajiamini zaidi katika uendeshaji wao na pia katika maandalizi.”

Jumla ya magari saba ya R5 yatawania taji la Equator Rally nchini Kenya mnamo Aprili 24-25. Idadi hiyo ya R5 ni kubwa kuwahi kushuhudiwa kwenye ardhi ya Kenya.

Equator Rally, ambayo inarejea baada ya kutofanyika kwa zaidi ya miaka 15, itatumiwa kama mashindano mawili katika shindano moja. Mbali na kuwa ni duru ya Bara Afrika, Equator Rally pia ni duru ya Mbio za Magari za Kitaifa za Kenya (KNRC) zinazodhaminiwa na benki ya KCB. Itaandaliwa Aprili 24-25.

Isitoshe, Equator Rally itatumiwa kama mashindano ya majaribio ya duru ya Mbio za Magari za Dunia (WRC) ya Safari Rally ambayo inarejea kwenye kalenda ya dunia (FIA) baada ya miaka 19 hapo Juni 24-27.

Dereva bingwa wa kitengo cha KNRC cha 2WD Wayne Fernandes anaamini kuwa idadi hiyo ya magari ya R5 ni ishara kuwa timu zinajiimarisha mapema.

“Kiwango cha chini sasa kimepandishwa. Nasubiri kwa hamu kubwa kuona jinsi magari ya R5 yatashindana dhidi ya ujuzi wa hapa nyumbani, kisha bila shaka vijana wetu dhidi ya madereva wa kigeni. Ni kitu kizuri kuwa tutatumia barabara zitakazotumiwa kwa Safari Rally tunapolenga kuweka akilini jinsi mambo yatakavyokuwa katika mashindano ya dunia pamoja na ushindani unaotarajiwa kutoka kwa magari ya R5. Nimegundua kuwa barabara huwa na kitu kipya kutokana na mabadiliko ya hali ya anga hapa nchini. Lazima kuwe na kitu tofauti – shimo lenye tope ama kisiki katika sehemu unayofaa kuwa muangalifu. Kwa hivyo niko na hakika kuwa kati ya mashindano ya Equator Rally na Safari Rally kuna kitu kitaongezwa barabarani,” alisema Fernandez.

Ndugu kutoka timu ya Kabras Sugar Racing Tejveer na mdogo wake Onkar wanatarajiwa kuendesha magari ya Volkswagen Polo R5.

Dereva mwingine Mkenya atakuwa na gari la R5 ni nyota Karan Patel atakayekuwa akijaribu bahati katika Ford Fiesta R5.

Amaanraj Rai, ambaye awali alishindana humu nchini, ameingia Equator Rally akiwa na leseni ya Uganda. Ataelekezwa na Oslaj Viljem kutoka Slovenia katika gari la Ford Fiesta R5.

Muingereza Pratul Ghose pamoja na mwelekezi wake mkazi wa Uingereza Mkenya Imran Khan watashirikiana katika gari la Minti Motorsport Volkswagen Polo R5.

Wakenya Aakif Virani na Azhar Bhatti wataendesha gari la zamani la bingwa wa Afrika Mkenya Manvir Baryan, Skoda Fabia R5.

Raia wa Afrika Kusini Guy Botterill na Simon Vacy-Lyle wamejiandikisha kutumia Toyota Etios R5.

Katika masuala ya kimataifa ya mbio za magari, R5 inamaanisha aina ya magari yanayoshindana chini ya masharti ya Kundi R. Magari ya R5 yako chini ya yale ya WRC katika nguvu na utendakazi. Yanakubaliwa kushiriki WRC katika vitengo vya WRC2 na WRC3.

WRC2 ni ya madereva wanaolenga siku moja kushiriki kiwango cha juu kabisa (WRC). Ni kitengo cha timu zinazoungwa mkono na kampuni zinazotengeneza magari wanayoendesha na timu binafsi zilizoidhinishwa na Shirikisho la Mbio za Magari Duniani (FIA).

Kitengo cha WRC3 kina masharti sawa na WRC2, lakini ni madereva binafsi pekee.

Wakati huo huo, mtaalamu wa kuchora barabara za Safari Rally Gurvir Bhabra amesema kuna vitu kadhaa kwenye barabara ya Equator Rally vitakavyosisimua washiriki.

Gurvir amethibitisha kuwa Equator Rally itakuwa na mikondo sita ambayo ni Elementaita, Soysambu, Sleeping Warrior, Loldia, Malewa na Sleeping Warrior.

Mikondo ya Safari Rally ambayo imeachwa nje ni Kasarani Super Special Stage (SSS), Oserian na Hell’s Gate (Wolf Power Stage).

Duru nyingine za Afrika baada ya Equator Rally ni Tanzania (Julai 24-25), Pearl of Africa Uganda (Agosti 21-22), Zambia (Septemba 25-26) na Afrika Kusini (Novemba 6-7).

Orodha ya washiriki wa ARC Equator Rally:

1 Eric Bengi-Peter Mutuma (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

2 Tejveer Rai-Gareth Dawe (Kenya) Volkswagen Polo-R5

3 Ian Duncan-Tej Sehmi (Kenya) Nissan 240RS -Classic

4 Carl Tundo-Tim Jessop (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

5 Onkar Rai (Kenya)-Drew Sturrock (Uingereza) Volkswagen Polo -R5

6 Baldev Chager-Ravi Soni (Kenya) Mitsubishi Evolution 10 RC2-R4

7 Karan Patel-Tauseef Khan (Kenya) Ford Fiesta -R5

8 Jasmeet Chana-Ravi Chana – Mitsubishi Evolution 10

9 Issa Amwari-Job Njiru (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

10 Amaanraj Rai (Uganda)-Oslaj Viljem (Slovenia) Ford Fiesta R5

11 Giancarlo Davite-Sylvia Vindevogel (Rwanda) Mitsubishi Evolution 10

12 Pratul Ghose (Uingereza)-Imran Khan (Kenya) Volkswagen Polo

13 Rajiv Ruparelia-Enoch Olinga (Uganda) Volkswagen Polo/Proto

14 Yasin Nasser-Ali Katumba (Uganda) Subaru Impreza

15 Duncan Mubiru-Musa Nsubuga (Uganda) Subaru Impreza

16 Kepher Walubi-Muhamadi Asuman (Uganda) Mitsubishi Evolution 10

17 John Ng’ang’a-Edward Ndukui (Kenya) Subaru Impreza

18 Nikhil Sachania-Deep Patel (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

19.Aakif Virani-Azhar Bhatti (Kenya) Skoda Fabia R5

20 Piero Canobbio -TBA (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

21 Hassan Alwi (Uganda)-James Mwangi (Kenya)Subaru Impreza

22 Mcrae Kimathi-Shameer Yusuf (Kenya) Subaru Impreza

23 Steve Mwangi-Dennis Mwenda (Kenya) Subaru Impreza

24 Guy Botterill-Simon Vacy-Lyle (Afrika Kusini) Toyota Etios RC2-R5

25 Christakis Fitidis (Uganda)-Eric Nzamwita (Rwanda) Mitsubishi Evolution 10

26 Hussein Malik l-Linet Ayuko – Mitsubishi Evolution 10

27 Evans Kavisi-Absolom Aswani (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

28 Ronald Sebuguzi-Anthony Mugambwa (Uganda) Mitsubishi Evolution 10

29 Jonathan Somen-Richard Hechle (Kenya) Ford Escort MK2 Classic

30 Kailesh Chauhan-Tariq Malik (Kenya) Ford Escort RS -Classic

31 Edward Maina-John Ngugi (Kenya) Subaru Impreza

32 Nzioka Waita-Tuta Mionki (Kenya) Mitsubishi Evolution 10

33 Daren Miranda-Wayne Fernandes (Kenya) Subaru Impreza RC2

34 Geoff Mayes-Suzanne Zwager (Kenya) Landrover Tomcat

35 Hamza Anwar-Riyaz Ismail (Kenya) Subaru Impreza

  • Tags

You can share this post!

Uozo wa kimaadili miongoni wa wabunge waanikwa

MAPISHI: Kuku kienyeji