• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 6:50 AM
Fraser-Pryce, Mkenya Imali kukabiliana Kip Keino Classic

Fraser-Pryce, Mkenya Imali kukabiliana Kip Keino Classic

Na AYUMBA AYODI

BINGWA wa Olimpiki na Dunia Shelly-Ann Fraser-Pryce kutoka Jamaica na Mwamerika Sha’Carri Richardson wametiwa katika makundi tofauti kwenye shindano la Kip Keino Classic mnamo Mei 13 mjini Nairobi.

Fraser-Pryce, ambaye alikosa shindano la Botswana Golden Classic mnamo Aprili 29 kwa sababu za kifamilia, atatetea taji la mbio za mita 100 naye Richardson atatimka 200m.

Uga wa kimataifa wa Moi Kasarani kwa mara nyingine utakuwa mwenyeji wa shindano la Kip Keino Classic ambalo ni la Shirikisho la Riadha Duniani la Continental Tour kiwango cha dhahabu.

Bara Afrika sasa ina mashindano mawili ya Continental Gold Tour baada ya Botswana kujumuishwa.

Msimamizi wa Kip Keino Classic, Barnaba Korir amesema kuwa Fraser-Pryce anayejivunia mataji 10 ya dunia yakiwemo matano ya 100m, amethibitisha kushiriki licha ya kujiondoa kwenye shindano la Gaborone.

“Tunafurahia kuwa watimkaji hawa matata wa mbio fupi watakuwa hapa, wakiongeza idadi ya mastaa, huku Richardson akitarajiwa kushiriki kwa mara ya kwanza,” akasema Korir.

Richardson alitimka katika 200m nchini Botswana na kukamata nafasi ya pili kwa muda wake bora msimu huu wa sekunde 22.54 baada ya Mwamerika mwenzake Kayla White kushinda taji kwa 22.38.

Hapo awali, Fraser-Pryce alitaka mashabiki wa Kenya wajitokeze kwa wingi kumtazama akitifua vumbi.

Fraser-Pryce almaarufu Mommy Rocket kwa mara nyingine atafungua msimu wake barani Afrika anakotarajia kuandikisha kasi ya juu.

Alitawala Kip Keino Classic kwa sekunde 10.67. Alimlemea Hemida Bassant kutoka Misri aliyekamilisha kwa sekunde 11.02.

Wapinzani wa Fraser-Pryce ni pamoja na bingwa wa dunia wa 4x100m Twanisha Terry na mshindi wa medali ya fedha ya Olimpiki 4x100m Daniels Teahna kutoka Amerika, na bingwa wa Kenya mbio za 100m na 200m Maximilla Imali.

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Pasta adaiwa kuua mkewe na kutuma mwanawe kumfahamisha chifu

Mbunge asema aliolewa akiwa kimwana bikira

T L