• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
Giroud awaaga Chelsea kwa shukrani tele akiungana na Tomori AC Milan

Giroud awaaga Chelsea kwa shukrani tele akiungana na Tomori AC Milan

Na MASHIRIKA

MSHAMBULIAJI matata raia wa Ufaranza Olivier Giroud amewashakuru mashabiki, wachezaji na makocha wa Chelsea kwa muda murua walioishi pamoja, anapoagana nao kuelekea AC Milan.

Giroud aliwasakatia Chelsea jumla ya michuano 119 na kuwafungia mabao 39, na kuwaongoza kunyakua mataji ya Klabu Bingwa Ulaya(Uefa Champions League), Taji la Uropa na kombe la FA.

“Naanza safari yangu mpya kwa mwangaza na raha moyoni. Kunyakua mataji ya Klabu Bingwa Ulaya, Uropa na FA imekuwa heri kubwa. Shukrani zangu ziwaendee mashabiki, wachezaji na umeneja,” alisema Giroud kupitia mtandao wa twitter.

Giroud, 34, ambaye alijiunga na Chelsea Januari 2018 kutoka Arsenal, alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake.

Nafasi yake ilikuwa finyu baada ya kutua kwa mastraika wa Ujerumani Kai Havertz na Timo Werner, akianza jumla ya mechi nane pekee za ligi kuu ya EPL.

Alihusishwa katika kikosi cha Ufaranza kwenye dimba la Euro 2020, ambapo walibanduliwa na Uswisi katika hatua ya 16-bora.

Kwa mujibu wa ripoti ya Sky Sports, alitua kwenye Kliniki ya La Madonnina mjini Milan Ijumaa kwa vipimo vya kimatibabu. Anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka miwili na kulipwa kima cha Euro 1milioni.

Milan pia waamemsaini difenda Fikaye Tomori, baada ya kuwa naye nusu ya msimu jana kwa mkopo.

AC Milan walitamatisha msimu jana katika nafasi ya pili na wanatarajiwa kuanza msimu ujao Agosti 22, watakapokwaruzana na Sampdoria ugenini.

TAFSIRI NA: NDUNGI MAINGI

You can share this post!

Mfumaji Lukas Nmecha ajiunga na Wolfsburg ya Ujerumani

Beki William Saliba ajiunga na Marseille naye Hector...