• Nairobi
  • Last Updated June 14th, 2024 7:55 PM
Beki William Saliba ajiunga na Marseille naye Hector Bellerin akiomba kuondoka ugani Emirates

Beki William Saliba ajiunga na Marseille naye Hector Bellerin akiomba kuondoka ugani Emirates

Na MASHIRIKA

BEKI William Saliba wa Arsenal amejiunga na Olympique Marseille ya Ufaransa kwa mkopo katika juhudi za kupata jukwaa zuri la kujikuza zaidi kitaaluma.

Nyota huyo aliyekuwa akiwaniwa pakubwa na Tottenham Hotspur, alisajiliwa na Arsenal kutoka Saint-Etienne ya Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kwa kima cha Sh4.2 bilioni.

Kuondoka kwa Saliba uwanjani Emirates kunafanyika saa chache baada ya beki matata raia wa Uhispania, Hector Bellerin kutaka Arsenal wamwachilie ayoyomee Italia kuvalia jezi za Inter Milan.

Baada ya kurasimisha uhamisho wake hadi Arsenal, Saliba alirejea Saint-Etienne kwa mkopo mnamo 2019-20 kabla ya kupokezwa jezi nambari nne baada ya kurejea London Kaskazini.

bali na kutojumuishwa katika kikosi cha wachezaji 25 waliotegemewa na Arsenal kwenye Europa League mnamo 2020-21, Saliba hakuchezeshwa pia katika mchuano wowote wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Alitumwa kwa mkopo hadi Nice ya Ufaransa mnamo Januari 2021 na akawajibishwa mara 22 kambini mwa kikosi hicho.

Saliba, 20, sasa anaungana aliyekuwa kiungo mwenzake kambini mwa Arsenal, Matteo Guendouzi, aliyesajiliwa na Marseille mwanzoni mwa Julai 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Giroud awaaga Chelsea kwa shukrani tele akiungana na Tomori...

Vissel Kobe, Sagan Tosu waokota alama Ligi Kuu Japan