• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Guinea na Mali zafuzu kwa fainali za AFCON kutoka Kundi A

Guinea na Mali zafuzu kwa fainali za AFCON kutoka Kundi A

Na MASHIRIKA

BAO kutoka kwa Seydouba Soumah dhidi ya Mali lilitosha kuwapa Guinea tiketi ya kufuzu kwa fainali zijazo za Kombe la Afrika (AFCON) zitakazoandaliwa nchini Cameroon mnamo 2022.

Goli hilo lililojazwa kimiani na fowadi huyo wa Partizan Belgrade ya Serbia katika dakika ya 75, liliwavunia Guinea ushindi muhimu wa 1-0 dhidi ya Mali ambao ni viongozi wa Kundi A.

Ina maana kwamba Guinea na Mali kwa sasa wamefuzu kwa fainali za AFCON zitakazosakatwa kati ya Januari na Februari 2022 baada ya kuahirishwa mwaka huu wa 2021 kwa sababu ya corona.

Namibia na Chad ambao walikuwa washindani wengine wa Kundi A hawakucheza mechi yao baada ya Chad kupigwa marufuku na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) kutokana na hatua ya serikali kutatiza uendeshaji wa shughuli za Shirikisho la Soka la Chad.

Ingawa Namibia walipewa ushindi wa bwerere wa 3-0 dhidi ya Chad, bado wasingweza kukamilisha kampeni za Kundi A mbele ya Guinea au Mali.

Namibia kwa sasa watacheza dhidi ya Guinea mnamo Machi 28, siku ambapo Mali nao watapokezwa ushindi wa bure wa mabao 3-0 katika mechi iliyokuwa iwakutanishe na Chad.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mpango wa MKU kujenga hospitali ya kisasa

Kang’ata awataka Wakenya wawe makini kipindi hiki...