• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 5:50 AM
Hamza Anwar aanza Mbio za Magari Uswidi bila nuksi

Hamza Anwar aanza Mbio za Magari Uswidi bila nuksi

NA GEOFFREY ANENE

DEREVA Mkenya Hamza Anwar ana kibarua kigumu cha kuridhisha katika raundi ya kwanza ya Mbio za Magari za Dunia (WRC) baada ya kumaliza siku ya kwanza bila mikosi, lakini katika nafasi ya mwisho nchini Uswidi, Alhamisi.

Akielekezwa na Adnan Din katika gari la Ford Fiesta R3, Anwar, 24, alimaliza mkondo wa Shakedown uliojumuisha kilomita 5.45 katika eneo la Hakmark katika nafasi ya 51 kwa jumla na nambari tisa (pia mwisho) katika kitengo cha chipukizi (JWRC) kwa dakika 4:09.9.

Bingwa wa dunia 2022 Kalle Rovanpera akishirikiana na Jonne Halttunen katika gari la Toyota GR Yaris R1, na Esapekka Lappi/Janne Ferm (Hyundai i20N R1) kutoka Finland walifagia nafasi mbili za kwanza kwa dakika 2:50.9 na 2:51.0 mtawalia naye Takamoto Katsuta/Aaron Johnston (Toyota GR Yaris R1) wakafunga tatu-bora kwa 2:51.2.

Baada ya siku ya kwanza, madereva tisa wanaoshiriki JWRC walipata ushauri kutoka kwa meneja wa kampuni ya magurudumu ya Pirelli, Terenzio Testoni. Mashindano rasmi yataanza Februari 10 na kufika kilele Februari 12. Anwar anawakilisha Kenya na Afrika. Aliibuka bingwa wa Afrika wa chipukizi mwaka jana.

  • Tags

You can share this post!

Wanasiasa walioshindwa uchaguzini bado wavuna nyadhifa...

Cristiano Ronaldo acheka na nyavu mara nne na kupitisha...

T L