• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 4:40 PM
Ibrahima Konate katika orodha ya wanasoka watano watakaosajiliwa na Liverpool

Ibrahima Konate katika orodha ya wanasoka watano watakaosajiliwa na Liverpool

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL wameordhesha wanasoka watano wanaolenga kusajili mwishoni mwa msimu huu ili kujisuka upya kwa minajili ya muhula ujao wa 2021-22.

Kati yao ni beki matata wa RB Leipzig, Ibrahima Konate, 21, na Ozan Kabak.

Konate ambaye ni tegemeo kubwa katika kikosi cha chipukizi wa U-20 nchini Ufaransa hata hivyo ataagana na Leipzig iwapo Liverpool wataweka mezani kima cha Sh4.8 bilioni.

Liverpool pia wamefichua mpango wa kumpa Kabak, 21, mkataba wa kudumu baada ya kipindi cha mkopo wa sogora huyo raia wa Uturuki aliyesajiliwa kutoka Schalke ya Ujerumani mnamo Januari 2021 kutamatika rasmi.

Iwapo watashawishika kufanya hivyo, basi mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) watalazimika kuweka mezani kima cha Sh2.5 bilioni kwa minajili ya maarifa yake.

Kufikia sasa, Kabak amechezeshwa na Liverpool mara tano ligini na akawa sehemu ya michuano yote ya mikondo miwili iliyoshuhudia Liverpool wakidengua Leipzig kwenye hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Konate alisalia benchi wakati wa mechi zote mbili zilizoshuhudia Liverpool wakifunga Leipzig jumla ya mabao 4-0.

Sogora huyo kwa sasa ni sehemu ya kikosi cha Ufaransa kinachoshiriki kampeni za Euro U-21. Ingawa aliachwa nje ya kikosi kilichopigwa 1-0 na Denmark, aliunga kikosi cha Ufaransa kilichopepeta Urusi 2-0 mnamo Machi 29, 2021.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Ujerumani, Italia na Uswidi watamba katika mechi zao za...

Jeraha kumnyima Lewandowski fursa ya kuongoza Poland dhidi...