• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 10:50 AM
KCB, Kabras wabomoa wapinzani, Monks na Machine wakiduwaza Homeboyz na Mwamba

KCB, Kabras wabomoa wapinzani, Monks na Machine wakiduwaza Homeboyz na Mwamba

NA GEOFFREY ANENE

KCB na Kabras Sugar wamedumisha rekodi zao za kutoshindwa kwenye Ligi Kuu ya raga nchini (Kenya Cup) baada ya kupepeta Menengai Oilers 62-15 na Strathmore Leos 47-6 mtawalia, Jumamosi.

Wanabenki wa KCB walishinda mechi yao ya tisa mfululizo kwa alama ya bonasi baada ya kutoka chini alama tatu na kuyeyusha Oilers kupitia miguso ya Samuel Asati (miwili), Brian Wahinya (miwili), Festus Shiasi (mitatu), Elphas Adunga, Andrew Amonde, Peter Waitere naye Darwin Mukidza akachangia mkwaju minne na penalti moja.

Oilers, ambao walilemewa na Kabras katika fainali msimu 2021-2022, walikuwa wa kwanza kuona lango la KCB kupitia penalti ya Geoffrey Ominde katika mechi hiyo ambayo wenyeji hao kutoka Nakuru walijipata chini 24-3 wakati wa mapumziko. Oilers ya kocha Gibson Weru ilijipata nyuma 50-3 kabla ya kupunguza mwanya huo hadi 50-10 kupitia mguso ulioandamana na mkwaju. Ominde alifungia Oilers mguso wa pili baada ya KCB kuimarisha uongozi wake hadi 55-10 kabla ya Waitere kuhitimisha.

Kabras pia walitoka chini 3-0 wakizamisha Strathmore kupitia kwa miguso ya Eugene Sifuna (miwili), Dan Angwech, Mathias Osimbo na Jone Kubu naye Ntabeni Dukisa akatinga mikwaju minne.

Katika michuano mingine iliyosakatwa Jumamosi, Monks ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki iliduwaza Homeboyz 20-19, wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Masinde Muliro wakazimwa 27-23 mjini Kakamega na Nakuru, Kenya Harlequin wakabomoa Blak Blad ya Chuo Kikuu cha Kenyatta 36-6 ugani RFUEA, nao Mean Machine wa Chuo Kikuu cha Nairobi wakanyamazisha Mwamba 22-18.

  • Tags

You can share this post!

WALIOBOBEA: Uhuru alipewa jina hilo na Mwai Kibaki

Thiago Silva sasa kuchezea Chelsea hadi Julai 2024

T L