• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 1:14 PM
Kenya Lionesses yaimarisha mazoezi kwa mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia

Kenya Lionesses yaimarisha mazoezi kwa mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia

Na GEOFFREY ANENE

TIMU ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande ya kinadada maarufu kama Kenya Lionesses imeimarisha matayarisho yake ya mechi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2022 dhidi ya Colombia.

Vipusa hao wa kocha Felix Oloo na Mitch Ocholla watalimana na Afrika Kusini mnamo Agosti 12 na Agosti 16 mjini Stellenbosch katika mechi za kujipima nguvu.

Hii itakuwa mara ya kwanza Kenya na Afrika Kusini zitaonana uso kwa macho tangu Kombe la Afrika mwaka 2019 wakati Lionesses ilipondwa 39-0 ikimaliza ya pili nyuma ya Afrika Kusini na mbele ya Uganda na Madagascar.

Afrika Kusini ilijikatia tiketi ya moja kwa moja kushiriki dimba la dunia litakalofanyika nchini New Zealand, huku Kenya ikipata fursa nyingine ya kuwania tiketi kama nambari mbili.

Lionesses ilicheza michuano miwili ya kujipima nguvu dhidi ya Madagascar mwezi Julai bila nyota wake wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji saba kila upande na kulipuliwa 27-10 (Julai 3) na 10-0 (Julai 11).

Nyota 12 wa raga ya wachezaji saba kila upande waliokuwa Olimpiki wataungana na kikosi hicho kinachojiandaa ugani KRU jijini Nairobi kabla ya kukutana na Colombia mnamo Agosti 25 ugani Nyayo.

  • Tags

You can share this post!

Water yazamisha Cereals Board ligi ya handiboli ya kinadada

Vigogo wanavyoviziana kuwania ubabe 2022