• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 10:50 AM
Kenya yapigia debe Tong-IL Moo-Do iwepo katika Olimpiki za 2028

Kenya yapigia debe Tong-IL Moo-Do iwepo katika Olimpiki za 2028

Na ABDULRAHMAN SHERIFF

KENYA kwa pamoja na shirikisho la Tong-IL Moo-Do duniani zinapigia debe mierekea ya Tong-IL Moo-Do ijumuishwe kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2028.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Clarence Ingalwa Mwakio wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Mombasa Open Tong-IL Moo-Do International Martial Arts yaliyofanyika katika ukumbi wa Aga Khan Academy ambapo nchi 16 zilishiriki.

Mwakio amesema mipango ya mchezo huo kujumuishwa katika Michezo ya Olimpiki inachukua muda mrefu kutokana na mambo yanayohitajika kukamilishwa kufuatwa. ‘Hatuwezi kuwa tayari kufikia michezo ya 2024 huko Paris lakini tunalenga 2028 na mipango tayari imeanza,’ alisema.

Anasema watatumia kipindi kati ya sasa na 2028 kuandaa mashindano zaidi ili kuishawishi Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuwa mchezo huo uko tayari kuwa katika programu ya Olimpiki.’Tumeanza kuzungumza na Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Kenya (NOC-K) kuhusu jsmbo hilo na tuna matumaini mskubes kamati hiyo itatusaidia kiksmilifu katika ajenda yetu hiyo,’ akasema.

Mwakio anasema pamoja na serikali kuisaidia timu ya Jasiri kikamilifu katika maandalizi na ushiriki katika mashindano hayo ya Mombasa Open, amefurahikia kuona wachezaji nao wamerudisha shukurani zao kwa kuhifadhi taji lao kwa miaka tisa mfululizo.

“Tunataka kuuendeleza ili Kenya izoe medali nyingi katika mashindano yote ya kimataifa,” akaongeza.Aidha, alifichua kwamba shirikisho hilo litapeleka mchezo huo katika shule za msingi na sekondari ili kuanza kuweka mizizi ya kupendwa na wanamichezo chipukizi nchini.

You can share this post!

Faki, Wanjiru imani wataunga timu ya taifa Hit Squad

Mdokezi aendelea kumwaga mtama kuhusu mauaji

T L