• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Kevin de Bruyne na Phil Foden washinda tuzo za Mchezaji Bora na Chipukizi Bora wa EPL mtawalia msimu huu

Kevin de Bruyne na Phil Foden washinda tuzo za Mchezaji Bora na Chipukizi Bora wa EPL mtawalia msimu huu

Na MASHIRIKA

KIUNGO Kevin de Bruyne wa Manchester City ametawazwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2021-22 huku mwenzake kambini mwa Man-City, Phil Foden akizoa tuzo ya Chipukizi Bora wa Msimu.

De Bruyne ambaye ni kiungo raia wa Ubelgiji, amefunga mabao 15 na kuchangia saba mengine. Ufanisi huo uliwezesha Man-City kutua kileleni mwa jedwali la EPL huku ikisalia mechi moja zaidi kabla ya kampeni za muhula huu kutamatika rasmi mnamo Mei 22, 2022.

“Kushinda tuzo hii kwa mara ya pili ni ufanisi ambao ninajivunia sana,” akasema De Bruyne.

Foden, 21, ndiye mchezaji wa kwanza kujizolea tuzo hiyo kwa misimu miwili mfululizo. De Bruyne, 30, alichaguliwa mshindi kwa wingi wa kura kutoka kwa umma kwenye tovuti ya EPL. Kura hizo zilijumuishwa na zilizotokana na manahodha 20 wa vikosi vya EPL na jopo la wataalamu wa soka.

Wanasoka wengine waliokuwa wakiwania tuzo ya Mchezaji Bora wa EPL msimu huu ni Joao Cancelo wa Man-City, Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold wa Liverpool, Jarrod Bowen wa West Ham United, Bukayo Saka wa Arsenal, Son Heung-min wa Tottenham Hotspur na James Ward-Prowse wa Southampton.

De Bruyne alijishindia taji hilo kwa mara nyingine mnamo 2019 na sasa anaungana na Thierry Henry, Cristiano Ronaldo na Nemanja Vidic ambao wamewahi kuzoa taji hilo zaidi ya mara moja.

Foden ambaye amefunga mabao tisa na kuchangia matano mengine kufikia sasa muhula huu, aliwapiku Alexander-Arnold wa Liverpool, Conor Gallagher anayechezea Crystal Palace kwa mkopo kutoka Chelsea, Tyrick Mitchell wa Palace, Mason Mount wa Chelsea, Aaron Ramsdale na Saka wa Arsenal na Declan Rice wa West Ham. Tuzo hiyo ya chipukizi hutolewa kwa mwanasoka aliye chini ya umri wa miaka 23.

Man-City walihifadhi taji la EPL msimu huu baada ya kukomoa Aston Villa 3-2 na kupandisha alama zao kutoka 90 hadi 93 moja pekee mbele ya Liverpool waliopiga Wolverhampton Wanderers 3-1 uwanjani Anfield.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kundi lataka wandani wa Raila na Ruto wazuiwe kugombea vyeo...

Muthama akwepa tena kampeni za Ruto Machakos kwa sababu ya...

T L