• Nairobi
  • Last Updated November 28th, 2023 6:55 PM
Kiambu Community FC yakuza vipaji vya soka na kuhimiza maadili mema ya kijamii

Kiambu Community FC yakuza vipaji vya soka na kuhimiza maadili mema ya kijamii

NA PATRICK KILAVUKA

Kiambu Community FC inapatikana uwanja wa Shule ya Msingi ya Kiambu. Imejengwa kwa msingi wa jamii usiokuwa na ukabila. Isitoshe, wanasoka ni wale waliojitokeza na njia moja tu kukuza talanta zao kuinua soka mashinani.

Mbali na kupambana ya nyendo ambazo zinazobomoa msingi wa wanajamii kupitia madawa za kulevya na visa visivyo adili.

Japo ilianzishwa mwaka wa 2014, imejipanga kukuza vipaji vya wanasoka chipukizi kuanzia wa umri mdogo kupitia akademia yake ya soka ya Blue Raiders Soka Academy.

Inakadriwa kwamba makinda wakisha chongwachongwa watapata nafasi ya kuwaweka katika vigezo vya kusakatia ngozi timu ya Community.

Timu hii ya wazima ina wachezaji wapatao 25. Ila, akademia ina chipukizi wa kuanzia miaka mitano.

Kudhihirisha inakata mizizi ya ukabila ina benchi ambayo inaongozwa mkufunzi Elijah Wekesa, timu meneja Bonface N. Gikura, katibu Adam Mbui mwekahazina Eluid Njuguna na daktari wake Charles Mbuthia Macharia.

Ina pia mashabiki kindakindaki ambao wanaifuata na kuitia motisha.

Japo inajitegemea kutokana na ukosefu wa ufadhili, wanajikakamua kushiriki ligi na vipute vya Kaunti ya Kiambu na Kanda ya Mlima Kenya.

Mwaka ilioasisiwa, ilishiriki Kombe la Governor’s Cup na kuibuka ya pili bora.

Wamewahi kushiriki dimba la Mradi wa Maendeleo ya Maeneo, Kiambu mwaka 2015. Miaka iliyofuata 2016 na 2017 ( wakijuliana kama Kiambu Arsenal) walishiriki Ligi ya Abardare Regional League (ARL) na kuibuka ya tano na saba mtawalia.

Mwaka huu, walikuwa wameanza kuwasha mataa Ligi ya Central League ( ARL) kwa kukandamiza timu ya White Eagles 1-0 uwanjani Kibichiku, Lower Kabete.

Kocha Wekesa alisema ufanisi wa timu umetokana na mnato wa kijamii ambao imeibua kwa kusaidiana kwa hali na mali pasi na kuegemea ukabila. Isitoshe, mazoezi makali, kujitia motisha mmoja na mwengine, kumakinika kwa wachezaji uwanjani na kurekebishana kwa heshima wakiisawazisha timu. Mbali na mawasiliano na kujulikana hali.

Anaongezea kwamba angependa kuipandisha daraja kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo hadi Ligi ya Supa Kitaifa.

Timu meneja Gikura anasema nia yake ni kuona timu inakua kila uchao mbali na kusaka ufadhili kuishika mkono ili, vipaji ambavyo vimekombolewa mavumbuni visiozea mitaani bali vinawiri na hata kunaswa na timu zingine.

Mfano wa wanasoka ambao wamelelewa na timu na kujiunga na Blue Raiders ambayo inashiriki Ligi ya Kaunti ya Kiambu ni madifenda Lawrence Kinyua, Benson Gitari na Sylvester Kihumba, kiungo George Ndungu, kiungo wavamizi Ikapel Olewa na Victor Mburu na fowadi David Kamau.

Daktari Macharia naye anasema kazi yake ni kuhakiksha wachezaji wote wako imara kiusuli na wako katika hali shwari kupiga soka.

Changamoto za timu ni vifaa vya michezo, usafiri na sare. Wanashukuru wahisani na mahabiki umbali timu imefika pamoja na motisha wanaoitia.

Miongoni mwa kikosi ni Isaac Ochieng, John Mwariri, Sylvester Kihumba, Lawrence Wanjohi, Victor Mburu, James Gichangi, Kennedy Olewa, Benson Kabera, Joseph Karanu, Stephen Njeri , John Nganga, Kelvin Shikuri, Peter Kidman Alex Njoroge na Muchema Njugi.

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Wandani wa Ruto Mlima Kenya wamemgeuka?

Simba SC yaelekea Afrika Kusini kurarua Kaizer Chiefs soka...