• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Kipa Buffon ajiunga upya na klabu ya Parma aliyoagana nayo miaka 20 iliyopita

Kipa Buffon ajiunga upya na klabu ya Parma aliyoagana nayo miaka 20 iliyopita

Na MASHIRIKA

KIPA veterani raia wa Italia, Gianluigi Buffon, amejiunga upya na kikosi cha Parma alichoagana nacho miaka 20 iliyopita.

Mlinda-lango huyo mwenye umri wa miaka 43 ametia saini mkataba wa miaka miwili na klabu ya Parma iliyompokeza malezi ya awali kabisa katika ulingo wa soka. Kikosi hicho kiliteremshwa ngazi kutoka Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mwishoni mwa msimu wa 2020-21.

Buffon aliagana rasmi na Juventus ya Italia mwishoni mwa msimu wa 2020-21 baada ya kuwajibikia miamba hao kwa awamu ya pili.

Kipa huyo alikuwa sehemu ya kikosi kilichonyanyulia Italia ubingwa wa Kombe la Dunia mnamo 2006 na amechezea timu hiyo ya taifa jumla ya michuano 176. Ndiye mwanasoka anayeshikilia rekodi ya kuwajibishwa katika michuano mingi zaidi ya Serie A (656) na alichezea Juventus mara 14 mnamo 2020-21.

“Tunafurahi kumkaribisha Buffon nyumbani. Kuja kwani ni jambo spesheli sana kwetu,” akasema rais wa Parma, Kyle Krause.

Buffon alichezea Parma kwa mara ya kwanza mnamo 1995 akiwa na umri wa miaka 17.

Tangu aagane na kikosi hicho mnamo 2001 na kuyoyomea Juventus kwa Sh3.3 bilioni – fedha zilizomfanya kipa ghali zaidi duniani wakati huo – amechezea klabu moja pekee nyingine tofauti.

Buffon alijiunga na Paris Saint-Germain (PSG) mnamo 2018 na akasaidia kikosi hicho kutwaa taji la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kabla ya kurejea Juventus mnamo 2019.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kevin de Bruyne atambisha Ubelgiji dhidi ya Denmark kwenye...

‘Plan B’ ya Kenya Shujaa baada ya ziara ya Los...