• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 9:50 AM
Kipchoge, Chepng’etich watoka bure tuzo ya mwanariadha bora duniani

Kipchoge, Chepng’etich watoka bure tuzo ya mwanariadha bora duniani

Na GEOFFREY ANENE

KENYA na Afrika nzima ilitoka mikono mitupu kwenye hafla ya kutuza wanariadha bora wa mwaka 2021 iliyofanyika nchini Ufaransa mnamo Jumatano usiku.

Mabingwa wa Olimpiki Eliud Kipchoge (marathon) na Faith Chepng’etich (mita 1,500) walikuwa katika orodha ya wawaniaji tano-bora wa tuzo ya mwanariadha bora mwanamume na mwanariadha bora mwanamke mtawalia.

Hata hivyo, mshikilizi wa rekodi ya dunia mbio za mita 400 kuruka viunzi Karsten Warholm kutoka Norway, ambaye alishinda kitengo hicho kwenye Olimpiki 2020 jijini Tokyo, na bingwa wa Olimpiki mbio za mita 100, mita 200 na mita 100 kupokezana vijiti (4×100) Elaine Thompson-Herah kutoka Jamaica waliibuka wanariadha bora mtawalia.

Bingwa wa mbio za mita 800 Riadha za Dunia Under-18 Emmanuel Wanyonyi pia aliambulia pakavu katika tuzo ya mwanariadha bora chipukizi sawa na Shirikisho la Riadha Kenya (AK).

Kwa jumla, Afrika haikupata tuzo yoyote kati ya 10 zilizopeanwa.

Wakenya ambao wamewahi kuibuka wanariadha bora duniani ni mshikilizi wa rekodi ya dunia mbio za mita 800 David Rudisha mwaka 2010 na Kipchoge mwaka 2018 na 2019 mtawalia.

You can share this post!

Wanasiasa wazimwa kushiriki harambee kuanzia Desemba 9

Hasira orodha ya mwisho ya kuwania tuzo ya fasihi ya...

T L