• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 8:50 AM
Kiungo Jack Wilshere kustaafu soka asipopata klabu ya kumsajili Januari 2022

Kiungo Jack Wilshere kustaafu soka asipopata klabu ya kumsajili Januari 2022

Na MASHIRIKA

KIUNGO wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza, Jack Wilshere amesema amewazia kwa kina kuhusu mpango wa kustaafu soka licha ya kuamini kwa asilimia 100 kwamba angali na uwezo mkubwa kutandaza soka.

Wilshere hajawahi kupata klabu mpya ya kujivunia huduma zake tangu aachiliwe na Bournemouth mnamo Mei 2021. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alirejea Arsenal anakochanganya mazoezi ndani ya kikosi cha kwanza na cha chipukizi wasiozidi umri wa miaka 23 pamoja na majukumu ya ukocha.

“Iwapo unatamani kuwa kocha bora, lazima upate tajriba pevu zaidi,” akatanguliza Wilshere ambaye hajawahi kunogesha mchuano wowote wa ushindani tangu atokee benchi na kuchangia ushindi wa 1-0 uliosajiliwa na Bournemouth dhidi ya Brentford mnamo Mei 17 katika mchuano wa mkondo wa kwanza wa mchujo wa Ligi ya Daraja ya Kwanza nchini Uingereza (Championship).

Wilshere anatarajia kujitosa upya katika ulingo wa usogora mnamo Januari 2022 ila hofu yake ni iwapo wepesi wa kupata mejaraha mabaya utamkosesha fursa ya kusajiliwa na kikosi chochote nje ya Uingereza. “Nimewazia kuhusu uwezekano wa kuangika daluga zangu.

Hiyo ndiyo sababu nilijitosa katika ukocha. Hii ni kazi ambayo ninaifurahia baada ya kupata fursa ya kuanza kujifunza polepole,” akaongeza Wilshere aliyechezea Uingereza mara 34. Aliwajibikia West Ham United na Bournemouth mara 36 tangu aagane na Arsenal mnamo 2018.

You can share this post!

Northern Ireland wasubiri Italia kwa hamu baada ya kukomoa...

JAMVI: ANC yatisha kujiondoa OKA ikiwa haitakuwa imeteua...

T L