• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 12:09 PM
JAMVI: ANC yatisha kujiondoa OKA ikiwa haitakuwa imeteua mgombeaji urais kufikia Desemba 25, 2021

JAMVI: ANC yatisha kujiondoa OKA ikiwa haitakuwa imeteua mgombeaji urais kufikia Desemba 25, 2021

Na CHARLES WASONGA

WANDANI wa kiongozi wa Amani National Congress (ANC) wametisha kuwa chama hicho kitajiondoa kutoka muungano wa One Kenya Alliance (OKA) ikiwa hautakuwa umetaja mgombeaji wa urais kabla ya Desemba 25, 2021.

RR RR by-Watatu hao walisema ikiwa OKA haitamtaja Bw Mudavadi kuwa mgombeaji urais wa muungano huo, ANC itajiondoa na kushirikiana na “marafiki wengine katika safari ya kuelekea Ikulu.”

“Tunawaambia wenzetu katika OKA kwamba tunataka kujua mgombeaji urais wa muungano huo kabla ya Desemba 25. Ikiwa mgombeaji huyo, ambae tunajua ni Musalia Mudavadi, hatatajwa basi sisi kama ANC tutaondoka ili tuunde muungano mwingine utakaomwezesha Musalia kupata urais,” Bw Mwale akasema.

Huku akiunga mkono kauli ya Mwale, Khamala alielezea imani kwamba Bw Mudavadi ataibuka mshindi ikiwa atapewa tiketi ya urais ya OKA. “Hatuamini kuwa OKA itashindwa katika uchaguzi mkuu ujao ikiwa itamteua Musalia Mudavadi kuwa mgombeaji wake wa urais. Hii ndio maana tunataka kujua mgombeaji wetu wa urais haraka iwezekanavyo,” akasema Khamala.

Naye Seneta Malala alisema, Wakenya wana hamu ya kujua mgombeaji urais wa OKA kwani “muda unayoyoma” “Kando na mgombeaji urais, Wakenya wanataka kujua nani atakuwa mgombeaji mwenza wa OKA ili waweze kufanya uamuzi bora debeni mwaka ujao,” akaeleza.

Kando na Mudavadi, vinara wengine wa muungano wa OKA ni Kalonzo Musyoka (Wiper) na Moses Wetang’ula (Ford Kenya) na mwenyekiti wa Kanu seneta Gideon Moi. Wote hao isipokuwa Bw Wetang’ula wametangaza azma ya kuwania urais na wamekuwa mbioni kujipigia debe ili wapewe tiketi ya kupeperusha bendera ya urais chini ya mwavuli wa muungano huo.

You can share this post!

Kiungo Jack Wilshere kustaafu soka asipopata klabu ya...

Serikali yahimizwa kubuni wizara ya masuala na mikakati ya...

T L