• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Kuandaliwa kwa Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili kutavuna pauni 3.3 bilioni zaidi

Kuandaliwa kwa Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili kutavuna pauni 3.3 bilioni zaidi

Na MASHIRIKA

KUANDILIWA na fainali za Kombe la Dunia kila baada ya miaka miwili kutavuna kipato cha ziada cha pauni 3.3 bilioni juu ya kile ambacho kimekuwa kikipatikana kwa kawaida kipute hicho kinapoandaliwa kila baada ya miaka minne.

Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limependekeza mabadiliko hayo kufanyika kama sehemu ya kuimarisha zaidi kampeni za kivumbi hicho. Ripoti kuhusu faida ya kubadilishwa kwa jinsi kivumbi hicho kinavyoandaliwa iliwasilishwa katika kikao kilichohudhuriwa na wanakamati 211 mnamo Disemba 21, 2021.

Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa), Ligi Kuu za bara Ulaya na Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (Conmebol) ni miongoni mwa wadau waliopinga mpango wa Kombe la Dunia kuandaliwa kila baada ya miaka miwili. Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) ni kati ya wadau ambao wameunga mkono pendekezo hilo.

Wajumbe waliohudhuria kikao cha Jumatatu waliambiwa kwamba fedha za kiingilio, haki za matangazo kupitia vyombo vya habari na udhamini iwapo kipute hicho kitafanyika baada ya miaka miwili zitaongezeka kutoka pauni 5.3 bilioni hadi pauni 8.6 bilioni kufikia 2030.

You can share this post!

Marudiano kwenye raundi za tatu na nne katika Kombe la FA...

Vipusa wa Arsenal wapewa Wolfsburg kwenye robo-fainali za...

T L