• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
KWPL: Ni mbio za farasi wawili, Gaspo Women na Vihiga Queens

KWPL: Ni mbio za farasi wawili, Gaspo Women na Vihiga Queens

NA AREGE RUTH

IMESALIA tu awamu ya mechi sita sita za Ligi Kuu ya Wanawake nchini (KWPL) kukamilika rasmi na ushindani mkali wa kutwaaa ubingwa wa ligi unaendelea kushika moto kati ya vinara Gaspo Women na Vihiga Queens.

Ni wazi kuwa, yeyote atakayelegeza kamba katika mechi zilizosalia atatemwa nje ya kinyang’anyiro hicho.

Gaspo wanaongoza kwenye msimamo wa ligi na alama 37,  mabingwa mara tatu wa ligi Vihiga wanafuata nafasi ya pili lakini wanatofautiana na mabao manne.

Katika mechi za awali tano, Gaspo wameshinda nne na kuandikisha sare moja. Vihiga wameshinda mechi zote tano.

Wikendi iliyopita mnamo Aprili 23, 2023, Gaspo walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Trans Nzoia Falcons katika uwanja wa Ndura mjini Kitale.

Wakati uo huo, Vihiga nao walitamba nyumbani ugani Mumias Sports Complex katika Kaunti ya Kakamega ambapo walipata ushindi finyu wa 1-0 dhidi ya Bunyore Starlets.

Timu hizi hazijakutana katika mchi ya mkondo wa pili. Mechi hiyo imepangwa kuchezwa mwishoni msimu huu wa 2022/23. Katika mechi ya mkondo wa kwanza Aprili 04, 2023, Gaspo walipata ushindi wa 2-0 ugani Mumias.

Wanajeshi wa Ulinzi Starlets, Wadadia Women na Nakuru City Queens wanafuata kwa nafasi za tatu, nne na tano mtawalia wakiwa na alama 32,31 na 29.

Juhudu za Thika Queens kutetea ubingwa wao msimu huu, zinaendelea kufifia baada ya kunyoroshwa 3-0 na Ulinzi Jumamosi iliyopita ugani Ulinzi Sports Complex jijini Nairobi. Walishuka hadi nafasi ya sita na alama 27.

Bunyore Starlets na alama (19), Kisumu All Starlets (17) na Zetech Sparks (16) wako  nafasi ya saba, nane na tisa mtawalia.

Mkiani nafasi ya 10 ni Trans Nzoia Falcons wana alama (16), Kangemi Ladies wanafuata nafasi ya 11 na alama (-3) Kayole wanafunga nafasi ya 12 na alama (-12).

Kayole waligoma kucheza mechi moja hata baada ya kufika uwanjani, wakakosa kusafiri kucheza mechi mbili za ugenini na wamepoteza jumla ya mechi 12 za ligi.

  • Tags

You can share this post!

Vifo: Serikali yaamka

DKT FLO: Nakerwa na hali ya mchumba wangu kukoroma anapolala

T L